Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, November 3, 2020

Mbowe na wenzake waachiwa kwa dhamana

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ni kati ya viongozi wa upinzani walioachiwa kwa dhamana leo Jumanne Novemba 3, 2020.

Wengine walioachiwa ni wajumbe wa kamati kuu ya Chadema,   Godbless Lema na Boniface Jacob ambao pamoja na Mbowe walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Novemba 2, 2020 wakiwa kwenye kikao. Zitto alikamatwa leo mchana alipokwenda kuwatembelea kina Mbowe polisi.


Wakili wa Chadema John Mallya amesema viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti polisi Novemba 5, 2020 saa 3 asubuhi.

Mallya amesema viongozi hao wameachiwa baada ya kujidhamini wenyewe na kutakiwa kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam na kuhakikisha wanaripoti kituoni hapo tarehe waliyopangiwa

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: