Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 5, 2020

Zitto Kabwe, Freeman Mbowe Waripoti Polisi


Mwenyekiti Chadema Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe pamoja na wajumbe watatu wa kamati kuu wameripoti kituo cha polisi Oysterbay na kutakiwa kuripoti tena kituoni hapo Jumatatu Novemba 9.

Wengine ni aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Chadema) Halima Mdee na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini Godbless Lema
 
Mbowe, Lema na Jacob  walikamatwa na polisi Novemba Mosi, 2020  huku Zitto akikamatwa Novemba 3, 2020 katika kituo cha polisi Oysterbay alikokwenda kuwajulia hali wenzake. Wote waliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti leo.

Mdee alijisalimisha polisi jana baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kumtaka kuripoti kwa mahojiano.

Leo viongozi hao waliwasili kituoni hapo kwa nyakati tofauti na kuelekea kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi na ilipofika saa 4:30 walitoka kwa pamoja.

Hata hivyo,  baada ya kutoka Mbowe hakutaka kuzungumza chochote badala yake aliagana na Zitto akieleza anarudi kituoni kwa ajili ya kufuatilia wafuasi wa chama hicho wanaoendelea kushikiliwa.


chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )