Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 23, 2020

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawashikilia Watu Sita Kwa Tuhuma Za Makosa Mbalimbali Ya Kiuhalifu Ikiwemo Mauaji


 Tukio La Kwanza
Tarehe 20.12.2020 Majira Ya 17:00hrs Huko Maeneo Ya Capripoint, Wilaya Ya Nyamagana, Mkoa Wa Mwanza, Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Lilimkamata  Benson Oluochi, Miaka 54, Mlinzi, Mkazi Wa Mtaa Wa Capripoint Kwa Tuhuma Za Kumuua  Mke Wake Aitwaye Elizabeth Benson, Miaka 45, Msukuma, Mjasiliamali, Mkazi Wa Capripoint, Chanzo Cha Tujkio Hili Ni Mtuhumiwa Kumtuhumu  Mkewe Kuwa  Hana Uaminifu Katika  Ndoa Alimshambulia Kwa Fimbo  Sehemu Mbalimbali Za Mwili Na Baadae Alipoteza Maisha  Muda  Mfupi Wakati Alipofikishwa Hospitali Ya Mkoa Sekou Toure Kwa Matibabu.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linakamilisha Uchunguzi Na Mtuhumiwa Atafikishwa Mahakamani Haraka Iwezekanavyo. Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa Hospitali Ya Mkoa Sekou Toure Kwa Uchunguzi Zaidi Wa Daktari

Tukio La Pili. Vita Dhidi Ya Dawa Za Kulevya

Tarehe 20.12.2020 Majira Ya 17:12hrs Huko Maeneo Ya Igombe A, Kata Ya Bugogwa, Wilaya Ya Ilemela, Mkoa Wa Mwanza, Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Lilimkamata   Sitta Gabunga, Miaka 66, Mkristo, Mjita, Mkazi Wa Igombe, Kwa Kosa La Kupatikana Na Dawa Za Kulevya Aina Ya Bhangi Kiasi Cha Gunia Tano Na Misokoto Thelathini, Ikikadiriwa Kuwa Na Uzito Wa Kilogramu 194, Kitendo Ambacho Ni Kosa La Jinai.

Tukio La Tatu. Misako Mikali Katikati Ya Jiji Na Wilaya Zote.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linaendelea Na  Misako Mikali Katikati Ya Jiji Na Wilaya Zote Za Mkoa Wa Mwanza Ambapo Watuhumiwa Sita  Wa Walikamatwa Na  Vitu Mbalimbali Vya Wizi.

Watuhumiwa Waliokamatwa Ni;-

    Raphael Sili, Miaka 25, Mkazi Wa Mahina, Mwendesha Pikipiki (Bodaboda)
    Seifu Said @rubengwa

    Isack Petro, Miaka 34, Mkazi Wa Kishiri

    Oscar Paul, Miaka 27, Mkazi Wa Igoma

Vitu Vilivyopatikana Ni;-

    Pikipiki Moja Yenye Namba Mc 971 Cdu Aina Ya Honlg Rangi Nyekundu.
    Tv Flat Screen Tatu Moja Aina Ya Hisense, Lg Na Nyingine Aina Ya Led.

    Tv Aina Ya Led Flat Screen
    Solar Aina Ya Sundar

    Radio Subwoofer Mbili Zote Aina Ya Seapiano.

 Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linaendelea Na  Mahojiano Ya Kina Na Watuhumiwa Pamoja Na Msako Mkali Katika Maeneo Yote Ili Kuweza Kubaini Na Kuwakamata Watu Wote Wanaojihusisha Na Vitendo Vya Kiuhalifu.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linatoa Wito Kwa Wananchi Hususani Wanandoa/watu Waliokua Kwenye Mahusiano Kuacha Tabia Ya Kujichukulia Sheria Mkononi Pindi Wanapokua Kwenye Migogoro, Bali Wafuate Taratibu Za Kisheria Na Kidini Ili Waweze Kusuluhishwa Kwa Amani. Vilevile Linaendelea Kutoa Wito Kwa Wananchi Kuendelea Kutoa Taarifa Zinazohusu Wahalifu Na Uhalifu Ili Zifanyiwe Kazi Kwa Haraka Na Watuhumiwa Waweze Kukamatwa Kabla Hawajatenda Makosa .

chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )