Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 23, 2021

Dorothy Semu Kaimu Mwenyekiti ACT Wazalendo


Chama cha ACT  Wazalendo kimemteua Dorothy Semu kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama hicho Kitaifa  kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa Chama hicho kitaifa Maalim Seif Hamad .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Salim A. Bimani amesema uteuzi huo ni kwa mujibu wa Ibara ya 84(3) na (4) ya Katiba ya ACT Wazalendo ya Mwaka 2015 Toleo la Mwaka 2020.

Ibara 84(3) imeeleza kuwa iwapo Mwenyekiti wa Chama hayupo kwa sababu yoyote ile, Makamu Mwenyekiti ambaye anatoka upande mwengine wa Muungano tofauti na anaotoka Mwenyekiti na kama makamu mwenyekiti aliyetajawa hayupo mwenyekiti aliyebaki atakaimu nafasi ya uenyekiti.

Aidha, kwa kuzingatia Ibara ya 84(4) ya Katiba ya ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu ataendelea kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12) hadi pale Mwenyekiti Mpya atakapochaguliwa na Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa.

Dorothy Semu kabla ya kukaimu nafasi hiyo alikuwa Makamu Mwenyekiti Bara  Chama cha ACT Wazalendo.


Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: