Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 5, 2021

Watumishi Waaswa Kulinda Hisia Zao Na Hisia Za Wengine Kuboresha Utendaji Kazi


Na Faraja Mpina – WMTH
Watumishi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wameaswa kulinda hisia zao na kuheshimu hisia za wengine ili kulinda amani, upendo, ushirikiano na kuongeza uwajibikaji mahali pa kazi na jamii kwa ujumla.

Hayo yamezungumzwa  na Mwezeshaji Jesse Mashami, wakati wa mafunzo juu ya utendaji kazi katika utumishi wa umma kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, jijini Dodoma

Mashami amesema kuwa watumishi wa umma wanapaswa kuthamini kazi walizonazo kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma katika utendaji wao.

“Linda hisia zako ili zisiathiri tabia na mienendo yako na kusababisha kutenda matukio yasiyostahili mahala pa kazi na kwenye jamii inayokuzunguka”, alizungumza Mashami

Aliongeza kuwa ni muhimu pia kuheshimu hisia za wengine kwa kuheshimu utu wao, kuwa wakarimu pamoja na kutambua na kusifia juhudi za wengine kwasababu kila binadamu ana njaa ya kutambuliwa na kusifiwa na wengine.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Zainab Chaula amewaasa watumishi wa Wizara hiyo kupendana, kuheshimiana na kuthaminiana kuanzia ndani ya vitengo na idara za Wizara hiyo ili kuongeza ari ya kufanya kazi na utekelezaji wa majukumu unaoridhisha.

“Sisi wote ni watumishi wa Serikali tunajenga nyumba moja, tuache fujo, tutembee pamoja kwa upendo na mshikamano katika kutimiza majukumu yetu kwa manufaa ya nchi na Serikali kwa ujumla”, Dkt. Chaula

Naye Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Muda Mfupi, Tafiti na Shauri za Kitaalamu Mhandisi Hosea George ametoa rai kwa watumishi hao kuhakikisha wanatoa mrejesho kwa wakati ili kusaidia utekelezaji wa majukumu na uendeshaji wa Wizara hiyo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: