Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, June 4, 2021

Waziri JAFO: " Takwimu za Wami Ruvu Zinaisaidia Serikali Kuchukua Tahadhari za Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi "


Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo, amesema  takwimu zinazotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu ni Muhimu kwa Sababu zimekuwa zikiisaidia Serikali hususani Wizara yake kuchukua Tahadhari kuhusu suala zima la Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye vyanzo vya maji ikiwemo Mito na Mabwawa.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo Mjini Dodoma kwenye  Wiki ya mazingira alipotembelea Banda la Maoensho la Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu.

Amesema Rasilimali maji ni Muhimu kwa maendeleo na Ustawi wa Binadamu, hivyo ameitaka Bodi hiyo ya Maji katika Bonde la Wami Ruvu kuwa mstari wa Mbele kuiongoza Serikali kupitia Takwimu zake ili iweze kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na athari za Mazingira kwenye vyanzo vya Maji.

“ Ofisi yenu ni muhimu sana, lakini inatusaidia vile vile kutoa tahadhari watu wasivamie vyanzo vya maji Kwa Sababu wakivamia Mambo yote yanakuja kuharibika, kwa mfano leo hii tunajenga lile bwana la Nyerere kama watu watavamia vyanzo vya Maji lile bwana litakuwa halijai ” Alisisitiza Wazir Jafo.

Kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani kinatarajia kufikia kilele chake June 5, ambapo Serikali inatarajia kuzindua Kampeni Kabambe ya Kuhamasisha Jamii Kutunza na Kulinda Mazingira.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: