Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, July 30, 2021

Kijana ajiteka ili apate fedha za kulipia madeni


Jeshi la Polisi Arusha linamshikilia Dickson Mungulu, aliyetuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wa taarifa za uongo kwa ndugu zake kwamba ametekwa na waliomteka wanahitaji milioni 3 wamuachie huru la sivyo watamuuwa, kumbe fedha hizo alikuwa akizihitaji ili alipe madeni.

Taarifa hiyo imetolewa  Julai 29, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo, ambapo amesema kuwa taarifa ya kijana huyo kutekwa ilitolewa Julai 25 kutoka kwa mmoja wa ndugu ambaye jina lake limehifadhiwa akieleza kuwa ndugu yao Dickson Mungulu, ametekwa.

Mara baada ya taarifa hiyo jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kisha kumkamata kijana huyo aliyesadikika kupotea na baada ya mahojiano walibaini kwamba mwaka 2020 alimaliza Shahada ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Makumira kilichopo Arusha.

Sambamba na hilo baada ya kumchunguza zaidi katika mwili wake ilibainika kuwepo na majeraha sehemu ya shingo na mguu alikiri kujichoma na kitu chenye ncha kali yeye mwenyewe kwa nia ya kuwaaminisha wazazi wake pamoja na ndugu zake wengine kwamba alitekwa.


Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: