Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, August 28, 2021

Naibu Waziri Bashe Aagiza Ukamataji Wa Mazao Shinyanga Usitishwe Mara Moja


 Na Faustine Gimu

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema mkoa wa Shinyanga unaenda kinyume na Maelekezo ya wizara kwa kukamata magari yanayobeba mazao ya dengu ,kunde na mbaazi hivyo wanatakiwa kuacha mara Moja kamatakamata hiyo .

Naibu Waziri huyo amesema kuanzia leo magari yote yaliyokamatwa katika mkoa wa Shinyanga yaachiwe mara Moja hivyo amesema kitendo hicho kinachofanywa na uongozi  wa mkoa wa Shinyanga ni Cha kibabe.

Aidha,Bashe amesema mwenye mamlaka ya kuagiza zao liuzwe kwa namna gani katika minada ni Waziri wa Kilimo pekee.

Ameongeza kuwa wafanyabiashara  Wana leseni lakini wanapofika katika mkoa wa Shinyanga wanakamatwa .

"Wafanyabiashara wamelipa ushuru Simiyu lakini wanakamatwa Tinde ,hatutaki namna hii"amesema.

Hata hivyo ,Bashe amesema halitajirudia lililotokea Shinyanga huku akiwapa pole wakulima pamoja na wafanyabiashara waliopata kadhia hiyo.

Zaidi ya Magari 30 ya mazao mbalimbali yalikamatwa mkoani Shinyanga kwa madai ya kutolipa ushuru wa mazao licha ya kulipa katika mikoa mingine

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: