Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, August 5, 2021

PICHA: Wafuasi Chadema wakamatwa Kisutu

Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuzuiwa kuingia ndani wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Wafuasi  hao waliokuwa wamefika kwaajili ya kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye hata hivyo hakufikishwa mahakamani walikamatwa baada ya kutoa mabango yenye jumbe mbalimbali na kuanza kuimba.

Baada ya wanachama hao kuanzisha nyimbo hizo, Polisi waliokuwa ndani ya magari wakiwa na silaha mbalimbali waliteremka na kuanza kuwakamata.

Kesi hiyo inayomkabili Mbowe na wenzake, ilikuwa inasikilizwa mahakamani hapo kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’, mbele ya Haki Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini baadae iliahirishwa  hadi kesho kutokana na tatizo la mtandao.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: