Ndugu
Wananchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa
kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2022.
Zoezi
hilo limehusisha jumla ya wanafunzi 907,802 wakiwemo Wasichana 467,967
na Wavulana 439,835 ambao ni sawa na asilimia 81.97 ya wanafunzi
waliofanya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2021. Kati ya
waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza wamo Wanafunzi
wenye mahitaji maalum 2,673 sawa na asilimia 0.29 ambao kati yao
wavulana ni 1,471 na wasichana 1,202.
Kwa
mwaka 2022 kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 73,932 sawa na asilimia
8.87 ya wanafunzi waliofaulu ukilinganisha na mwaka, 2020 ambapo jumla
ya wanafunzi 833,872 walifaulu na kupata sifa ya kujiunga na masomo ya
Kidato cha Kwanza.
_______
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )