Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, November 1, 2021

Rais Samia akutana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, jana tarehe 31 Oktoba, 2021 amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika masuala ya biashara kati ya Uingereza na Tanzania Lord  John Walney.

Bw. Walney amekutana na Mhe. Rais Samia kujitambulisha akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji na utalii.

Amesema kukutana kwake na Mhe. Rais Samia kumempa fursa ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania ambavyo vitamuwezesha kuwashawishi zaidi wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza katika sekta ya bishara na utalii nchini Tanzania

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Bw. Walney kwa uamuzi wake wa kukutana nae na kujitambulisha kwake na kumueleza kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Uingereza katika kuchochea biashara baina ya nchi mbili hizo.

Mhe. Rais Samia amesema Serikali ya Uingereza na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa kibiashara kwa muda mrefu ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi zinazoongoza kuwekeza nchini Tanzania, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi za kibiashara katika kukuza ushirikiano wa uchumi na Uingereza.

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: