Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, December 14, 2021

Akina Mbowe Wagonga Mwamba, Mapingamizi Yatupwa


Mahakama Kuu Devisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayohusu maelezo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa wa tatu katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, Mohamed Abdillah Ling’wenya, kufuatia pingamizi lililowekwa na mawakili wa mshtakiwa huyo, Fredrick Kihwelo na Dickson Matata.

Katika kesi hiyo ndogo mawakili hao wa mshtakiwa huyo walipinga kupokewa maelezo hayo akitoa hoja mbalimbali huku akiungwa mkono na mawakili wengine wa utetezi.

Pamoja na mambo mengine mawakili wa utetezi walipinga kupokewa maelezo hayo kwa madai kuwa mshtakiwa huyo hakutoa maelezo kituoni hapo, kwa kuwa hajawahi kufikishwa kituoni hapo na kwamba hakuwahi kutoa maelezo yake popote.

Mapingamizi hayo yametupiliwa mbali leo Jumanne Desemba 14, 2021 na Jaji Joachim Tiganga ambaye anasikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu amesema kuwa hoja zote za utetezi zimetupiliwa mbali hivyo maelezo haya yanapokewa.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: