Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 30, 2021

Mapigano ya wakulima na wafugaji yasababisha kifo na majeruhi Morogoro


Mapigano  yamezuka kati ya wakulima na wafugaji wilayani Malinyi mkoani Morogoro na kusababisha kifo cha mkulima mmoja na wengine sita kujeruhiwa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea katika mradi wa kilimo cha umwagiliaji uliopo kijiji cha Itete, akimtaja aliyepoteza maisha kuwa ni Abdul Said (34) mkazi wa Ifakara wilayani Kilombero.

Kamanda Muslim alisema tukio hilo limetokea Desemba 27 mwaka huu huku chanzo cha mapigano hayo ni baada ya vijana watatu akiwamo Abdul kuzuia mifugo iliyoingia katika mashamba hayo.

Alisema wakati vijana hao wakiendelea kuzuia mifugo hiyo ndipo yalipozuka mapigano baina yao na wafugaji hao, kwamba walizidiwa nguvu na kukimbilia kusikojulikana kisha mwili wa kijana huyo ulipatikana kesho yake usiku.

"Baada ya kutokea mapigano hayo wale wakulima walizidiwa nguvu, hivyo wakakimbia, Jeshi la Polisi Malinyi lilipopata taarifa lilianza jitihada za kuwatafuta bila mafanikio hadi ilipofika saa 9 usiku ndipo mwili huo ulionekana katika mashamba hayo," alisema Muslim.

Kamanda Muslim alisema kuwa baada ya mwili wa kijana huyo kupatikana akiwa amefariki baadhi ya wanakijiji walilazimisha uchunguzi wa kidaktari kufanyika hadharani, ndipo daktari alipofika na kuufanyia uchunguzi.

Aliendelea kueleza kuwa baada ya uchunguzi kukamilika daktari alishindwa kutoa majibu hadharani kwa sababu za kimaadili, ndipo wanakijiji hao wakaanza kuwashambulia kwa mawe daktari na askari waliokuwa sehemu ya tukio.

Kamanda Muslim alisema baada ya kutokea kwa hali hiyo Jeshi la Polisi lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanakijiji hao.

"Jeshi la Polisi lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanakijiji hao baada ya kuanza kurusha mawe kushinikiza ripoti ya uchunguzi wa daktari isomwe, baada ya kutawanyika baadae Jeshi la Polisi tulirudi kuangalia ndipo tukapata taarifa kuwa kuna makazi ya wafugaji 17 waliokuwa wakiishi jirani na mashamba hayo yamechomwa moto,” alisema Kamanda Muslim.

Alibainisha kuwa katika tukio hilo la uchomaji moto wa makazi hakuna madhara yeyote kwa binadamu yaliyotokea kwa sababu wafugaji hao walikuwa wameyakimbia makazi yao baada ya kuona kuna mkusanyiko mkubwa wa watu kijijini hapo.

Credit:Nipashe


 

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: