Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 8, 2021

Mradi Wa Julius Nyerere Kukamilika Bila Ongezeko La Gharama.


 Mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa megawati 2115 wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika bila ongezeko la gharama za ujenzi. Hayo yameelezwa na  Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba Desemba 7, 2021 alipotembelea eneo la mradi akiambatana na Waziri wa Nyumba Maendeleo ya Makazi na huduma wa Jamuhuri ya kiarabu ya Misri Mhe .Assem Hafez El azar.

Ziara hiyo ilikuwa ya pamoja kati ya  Nchi za Tanzania na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ambayo imepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi ya mwezi  Novemba  2021, inayoonesha kuwa  utekelezaji wa mradi unakwenda vizuri.

‘‘kwa dhamira na malengo ya mradi, na gharama zilizotumika, Serikali ya Tanzania haiwezi kuruhusu mradi huu kutokukamilika, kwa wenzetu wa Misri pia  mradi  huu ni chachu ya  ushirika yenye manufaa kwao pia  nao wako tayari kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa faida ya nchi zote mbili. ‘’ amesema Waziri Makamba.

Ameelekeza timu ya wataalam toka Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO kuangalia changamoto zilizojitokeza na kuzifanyia kazi ili kuhakikisha mradi unakamilika kama Mhe. Rais Samia Suluhu Hasan alivyowaahidi watanzania.

Naye Mhandisi Assem Hafez El azar, ambae ni Waziri wa Nyumba Maendeleo ya Makazi na Huduma wa Misri amesema, Serikali ya Misri inawahakikishia watanzania kuwa  mradi wa JNHPP ni muhimu kwa nchi zote mbili ili kujenga mahusiano na imani kwa watanzania kuwa misri ni Nchi nyenye uwezo wa kutekeleza miradi mingine mikubwa ambayo Tanzania itatazamia kuijenga.

Katika ziara hiyo Mhe. Makamba aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati, wa Tanzania Mhe. Stephen Byabato, Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande pamoja na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati ambao wamekagua  pia maeneo muhimu ya mradi  yanayoendelea kujengwa  ambayo ni nyumba ya mitambo, sehemu ya kupokelea umeme pamoja na eneo linapo jengwa daraja.

Kukamilika kwa wakati kwa mradi Julius Nyerere kutasaidia  Nchi kupata umeme wa uhakika, bora na wa gharama nafuu na hivyo kukuza uchumi sambamba na kuongeza ajira kwa wataalamu mbalimbali.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: