Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 30, 2021

Mwanamke Mwingine Auawa Jijini Arusha


Happy Lazaro, Arusha
Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro, jijini Arusha,Janerose Dewasi(66) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na anayetuhumiwa ni mfanyakazi wake wa ndani.


Tukio hili  limetokea siku chache baada ya mwanamke mwingine,Ruth  Mmasi kubainika kuuawa eneo la Njiro pia na anayetuhumiwa ni mtoto wake wa kiume Patrick Mmasi(19)


Kamanda wa  polisi mkoani Arusha,Justine Masejo amethibitisha kutokea mauwaji hayo kubainika leo saa 2:30 asubuhi na kueleza kuwa polisi  wanamsaka  mfanyakazi wa ndani ambaye anatuhumiwa baada ya kufanya mauwaji hayo alitoweka.


Kamanda Masejo amesema imebainika mwanamke huyo ambaye alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo kwenye nyumba yake eneo la block D mwili wake umepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso kushoto.


” uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo wao pekee na alimuajiri wiki moja iliyopita”amesema


Hata hivyo amesema mara baada ya mauwaji hayo mfanyakazi huyo ametoweka na anaendelea kusakwa.
Kamanda amesema jeshi la polisi linatoa wito kwa wenye nyumba kuwa makini na wafanyakazi wa ndani wanaowapa kazi kwa kujua historia zao.


Mmoja wa majirani wa nyumba hiyo,Mary Muchi alisema mfanyakazi huyo alikuwa hajulikani sana mtaani kwani ameanza kazi muda si mrefu.


“Hatujuwi lolote huyo kijana anatajwa boniface alikuwa akiimsaidia huyu mama kazi zao na leo tumeshangaa kupata taarifa za kifo cha mama huyu”amesema.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: