Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 29, 2021

Tangazo la Kuitwa Kwenye Mtihani wa Usaili wa Maandishi (Apptitude Test) - Kutoka TAKUKURU / PCCB


Mkurugenzi  Mkuu  wa Taasisi  ya  Kuzuia  na  Kupambana na  Rushwa (TAKUKURU) anapenda  kuwatangazia watu wote walioomba nafasi ya ajira ndani ya  Taasisi ya  kuzuia  na  Kupambana na  Rushwa kwamba  mtihani  wa usaili  wa maandishi  (apptitude test) utafanyika Jijini Dodoma siku ya tarehe 8.1.2022.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia

1.  Tarehe ya usaili ni tarehe 8.1.2022 siku ya Jumamosi;
2.   Kwa waombaji  ambao  wameomba  kazi ya  Afisa  Uchunguzi  mtihani  wao utaanza  saa 2:30 asubuhi siku hiyo tarehe 8.1.2022;
3.   Kwa  waombaji  ambao  wameomba  nafasi  ya  Uchunguzi  Msaidizi  mtihani wao utaanza  saa 6:00 mchana  siku hiyo ya tarehe 8.1.2022;
4.   Waombaji  walioitwa kwenye usaili huu wahakikishe  wanachukua  tahadhari zote  za kujikinga  na ugonjwa  wa  UVIKO-19  muda  wote wanaposafiri  na wanapokuwa kwenye chumba cha mtihani;
5.  Majina  ya  waombaji   wote  walioitwa  kwenye  usaili  pamoja   na  eneo  la kufanyia    mtihani     yanapatikana     kwenye     wavuti     ya    TAKUKURU wwww.pccb.go.tz;
6. Kila  mwombaji  ajaze  taarifa  zake  binafsi  kwenye  fomu  ambayo imeambatishwa  na orodha ya majina. Fomu pia inapatikana kwenye wavuti ya TAKUKURU   pccb.go.tz:
7.  Fomu ya taarifa binafsi  ijazwe  kwa umakini  na kwa usahihi.  Fomu  hiyo ni sehemu ya mtihani  wa apptitude test, kwa hiyo mtu  atakayejaza vibaya Fomu hiyo atakuwa ameipoteza nafasi ya kufaulu kwenye usaili huu;
8.   Fomu  hivo iwasilishwe  siku  ya  mtihani  tarehe  8.1.2022.  Msailiwa  ambaye hatawasilisha_Fomu_hio atahesabika kuwa ni miongoni mwa  walioshindwa kwenve usaili.
9,   Watakaofaulu  kwenye  mtihani   wa  maandishi  ndio  watakaoitwa  kwenye usaili wa mahojiano (oral interview)

Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa

==>>BOFYA HAPA KUPAKUA FOMU NA KUTAZAMA MAJINA

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: