Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 24, 2021

Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili :TCAA, BAKITA, CBE, NCT, MPRU, ATC, UDOM, STAMICO, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Utalii & Ofisi ya Waziri Mkuu


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Utalii cha Taifa (NCT), Bodi ya Wadhamini   ya Hifadhi   za Bandari na Maeneo Tengefu   (MPRU), Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), anapendakuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwakuanzia tarehe 08 - 10 Januari, 2022 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombajikazi watakaofaulu usaili.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i.      Usaili utafanyika   kuanzia tarehe 08-10 Januari, 2022 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili;  muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;

ii.     Usaili wa Mchujo (kuandika) kwa kada zote utafanyika tarehe 08 Januari, 2022 na usaili wa Mahojiano ya ana kwa ana utafanyika tarehe 10 Januari, 2022.

iii.   Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa, kunawa na sabuni kwa maji tiririka, kutakasa mikono, kuvaa mavazi rasmi yanayokubalika mahala pa kazi na pia inashauriwa kuvaa mavazi mazito kutokana na hali ya hewa ya ubaridi kwa kipindi hicho jijini Dodoma.

iv.    Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

v.   Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria; Msailiwa atakayekosa mojawapo ya kitambulisho kati ya vilivyotajwa hatoruhusiwa kuendelea na usaili;

vi.    Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;

vii. Wasailiwa watakaowasilisha Hati za Ushuhuda wa ushiriki mafunzo (Testimonials), Hati za Matokeo ya muda mfupi (Provisional Results), Taarifa za Matokeo (Statement of results), Hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;

viii.  Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;

ix.    Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

x.     Kwa waombaji      waliosoma    nje   ya   Tanzania   wahakikishe   Vyeti   vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);

xi.    Waombaji   kazi   ambao   majina   yao   hayakuonekana   katika   tangazo   hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.  Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

xii.  Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za
kufanyia kazi.

xiii.  Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

 

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: