Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 11, 2021

Wizara Yapongezwa Kutoa Elimu Maonyesho ya 21 ya Wajasiriamali wa Afrika Mashariki Jijini ,Mwanza


Na Daudi Manongi,Mwanza
Wananchi wa Jiji la Mwanza pamoja na waliotoka katika Mikoa mbalimbali na wale wa Afrika Mashariki wameendelea kutembelea banda  la Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na mabanda ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ambapo kwa nyakati tofauti wamepongeza huduma na elimu inayotolewa na wataalam   wa  Wizara   na Taasisi zake hususan juu ya  Majukumu ya Wizara hiyo yanayogusa Sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.Pongezi hizo wamezitoa katika viwanja vya Rock city mall jijini Mwanza ambao maonyesho ya 21 ya wajasiriamali wadogo na wa kati yanaendelea  ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara hiyo Bi.Hanna Churi  kutoka Singida amesema kuwa elimu aliyoipata kutoka kwenye banda la Wizara hiyo imewapa uelewa mpana kuhusu namna Mkongo  wa Taifa wa Mawasiliano unavyosaidia kupitisha na kusafirisha mawasiliano ya aina zote, ikiwemo huduma za intaneti, taarifa mbalimbali, picha za video na kuongea kwa simu kwa usikivu madhubuti.

“Kwa kweli nimefuraishwa sana na  huduma mnazotoa katika maonyesho haya nime elimika vya kutosha kwa kutembelea banda lenu na mmefanya jambo jema kwa kusogeza huduma  mbalimbali kwa wananchi  ” amesema Churi.

Kwa upande wake Bi Emilia James kutoka Arusha amesema amefurahishwa na taarifa alizopata kuhusu namna Mfumo wa Anwani  za Makazi na Postikodi unavyofanya kazi na kufahamu jinsi gani utawanufaisha wananchi katika maeneo yao.

Aidha kwa upande wa Ibrahim Chorwa Mkazi wa Mwanza amesema amevutiwa na majukumu mbalimbali ya Idara ya Habari-MAELEZO ikiwemo kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, Mipango na Miradi ya Maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi na kuipongeza Idara iyo kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Maonyesho ya 21 ya wajasiriamali wadogo na wa kati wa Afrika Mashariki  yalianza tarehe 2 Disemba na yatamalizika tarehe 12 Disemba 2021 jijini Mwanza

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: