CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye alijiuzulu tarehe 6 Januari mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa
habari tarehe 9 Januari, 2022 Visiwani Zanzibar, Katibu wa NEC-
Itikadi Uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka amesema mchakato huo utaanza
kuanzia tarehe 10 hadi 30 Januari mwaka huu.
Amesema hatua hiyo imekuja baada ya Ndugai kuandika barua kwa hiari yake na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM jijini Dodoma.
Amesema kufuatia hilo CCM
kinawatangazia wanachama wake wote kwamba utaratibu wa ratiba ya
mchakato wa kumpata mgombea atakayechaguliwa na wabunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujaza nafasi ys Spika wa Bunge.
Amesema utaratibu huo ni
kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
inayotambua Spika kuwa ndio kiongozi mkuu wa Bunge na nafasi hiyo
haiwezi kuwa wazi na Bunge likaendelea kufanya shughuli zake.
Akinukuu Katiba hiyo
amesema; Ibara ya 84 (i) kutakuwa na Spika ambaye atachaguliwa na
wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni wabunge au wenye sifa za kuwa
wabunge, atakuwa ndio kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika
vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.
“Ibara ya 84(viii) inasema
hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge isipokuwa uchaguzi
wa spika wakati wowote ambao kiti cha spika kipo wazi.
“Ibara ya 86(i) kimeeleza
kutakuwa na uchaguzi wa spika katika kikao cha kwanza cha mkutano wa
kwanza wa Bunge jipya, na katika kikao cha kwanza chochote mara baada ya
kutokea kiti cha spika kuwa wazi.
“Kwa minajili hiyo, katika
kutekeleza matakwa ya kikatiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,
nichukue fursa hii kwa niaba ya chama kutangaza kwamba mchakato wa
kujaza kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
utatekelezwa kwa ratiba ifuatayo sambamba na vikao vya mchujo na
uchaguzi wa wabunge wa CCM kabla ya kupelekwa bungeni kuendelea na
utaratibu mwingine,” amesema.
Amesema kuanzia tarehe 10
hadi 15 zoezi la kuchukua fomu litaanza rasmi na tarehe 15 ifikapo
alasiri zoezi hilo litakuwa limekamilika.
Amesema wale wenye sifa
alizotaja wanakaribishwa kuchukua fomu katika makao makuu ya chama ofisi
kuu, makao ya chama Dodom, ofisi ndogo Dar au Kisiwandui wakifika
watapata maelekezo namna ya kcuhukua fomu hizo.
Amesema tarehe 17 Januri,
2022 Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya Taifa itakutana kwa ajili ya
kujadili wagombea na kuishauri Kamati Kuu ya Halmashuri kuu ya Taifa juu
ya wagombea ambao wamejitokeza kuomba kiti hicho cha uspika.
“Tarehe 18 hadi 19 Januari
kutakuwa na kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho ambapo Kamati
kuu ya Halmashauri Kuu itafanya kazi hiyo kwa eneo ambalo litaelekezwa.
“Kuanzia tarehe 21 hadi 30
Januari katika siku hizo, cocus ya chama ya wabunge wa CCM itapiga kura
kumpata mgombea ambaye atakwenda bungeni kuomba kuchaguliwa kuwa Spika
wa Bunge la Tanzania,” amesema.
Amesema itategemea kama
mgombea atakuwa wa CCM au vyama vingine lakini kwa upande wa CCM
mchakato wake utakamilishwa na cocus ya CCM ambayo itampata mgombea
mmoja atakayepelekwa bungeni.
“Nichukue fursa hii
kuwataka watanzania wote ambao wanakidhi vigezo kwa mujibu wa katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na CCM, kwamba wana nafasi na wana fursa
kujaza nafasi hii,” amesema.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )