Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, January 21, 2022

Viongozi Watatu Chadema Manyara Washikiliwa Na Polisi


 Na John Walter-Manyara
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linawashikila Viongozi watatu wa CHADEMA kwa kosa la kufanya mkutano bila kibali katika eneo la Stendi ya Katesh wilayani Hanang.


Viongozi wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) mkoa wa Manyara Regula Mtei (45), Valentina Shayo (37) Mhasibu wa Bawacha mkoa wa Manyara na mjumbe wa Kamati tendaji BAWACHA wakifanya mkutano wa hadhara bila kibali.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga katika taarifa hiyo ya Januari 19.2022, imeeleza kuwa viongozi hao walifanya kosa hilo Januari 15 mwak huumajira ya saa tisa alasiri wilayani humo.
Taarifa hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii imeeleza kuwa baada yaviongozi hao  kukamatwa na kufikishwa kituoni walihojiwa na kukiri kosa lao na kwamba 17.1.2022  walifikishwa mahakamani.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: