Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 5, 2022

Watu 9 wamefariki katika ajali ya boti Zanzibar


Watu tisa wamefariki dunia na wengine kadhaa kuokolewa baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama Mkoa wa Kusini Pemba.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Matar Zahor Masoud amesema ajali hiyo imetokea  Jumanne Janauri 4, 2022 jioni wakati watu hao wakitokea Chakechake kwenda Kisiwa Panza msibani, moja ya vyombo vilivyotumika kuwavusha kimepata hitilafu na kuzama.

"Mpaka sasa maiti tisa zimeopolewa zipo hospitali ya Mkoani kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari ili baadaye taratibu za kukabidhi familia zao zitaendelea," amesema

"Kwahiyo kwa wenzetu wa vyombo vya ukozi kwa maana ya KMKM (Kikosi Cha kuzuai Magendo) na wananchi walikuwa wakiendelea na zoezi hili lakini kutokana hali ya maji na kiza kazi hiyo tumeiahirisha tutaendelea nayo asubuhi mapema sana kuangalia kama kuna maiti nyingine au watu walionusurika tuweze kuwaokoa" amesema

Amewaomba wananchi kutoa ushirikiano na kuendelea kuwa na uvumilivu Serikali itatoa taarifa zaidi baadaye.

Amesema hawajapata taarifa za chanzo cha ajali lakini taarifa za awali zinadai huenda ikawa ni idadi kubwa ya watu waliokuwa ndani ya boti hiyo kwasababu hakuna uhakika walikuwa watu wangapi lakini ni kwamba walikuwa wanazidi watu 30.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: