Rais wa China Xi Jinping atampokea mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mjini Beijing leo, ambapo viongozi hao wawili wanatarajiwa kuonyesha mshikamano mkubwa wakati mzozo kuhusiana na Ukraine ukiendelea kutokota.
Hadi sasa China imesimama na Urusi katika mzozo huo, ikisisitiza ulazima wa kuheshimiwa kwa maslahi ya kiusalama ya Urusi, na kupinga kupanuka kieneo kwa jumuiya za kijeshi kama NATO.
Putin amesafiri kwenda China kushiriki katika ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, ambayo imesusiwa na nchi za magharibi, zinazoituhumu China kukiuka haki za binadamu. Michezo hiyo inafunguliwa rasmi leo Ijumaa.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )