Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, March 19, 2022

Askari Polisi Watakiwa Kutumia Weledi Na Maadili Wanapotekeleza Majukumu Yao

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amewataka askari Polisi kote nchini kuendelea kutumia weledi, maadili na ushirikishwaji wa jamii wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Sagini amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa cheo cha Koplo wa Polisi katika Shule ya Polisi iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo jumla ya askari 1750 wamehitimu mafunzo hayo na kuwaagiza askari hao kwenda kuyashughulikia makosa ya uhalifu wa kimtandao ambapo baadhi yamekuwa yakidhalilisha Utu, Kuchochea chuki na uhasama katika Jamii zetu pamoja na kuathiri uchumi na kutishia amani, utulivu na usalama.

Hata hivyo, Naibu Waziri Sagini  ameuagiza Uongozi wa Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki za kuzuia uhalifu na kuwashughulikia wahalifu wote watakaobainika.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: