Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, April 28, 2022

Ajali Yaua Askari Polisi Wawili na Mahabusu Wawili


Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya kigaidi pamoja na mauaji, wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 katika Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Sengerema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la polisi aina ya Toyota Landcruise yenye namba za usajili PT 3798 lililokuwa likitokea mkoani Mwanza, kukata ‘sterling rod’ na kuhama kutoka upande wake na kwenda upande mwingine na kugongana na Lori aina ya Scania lenye tela namba. T.865 mali ya kampuni ya Nyanza Botling.

Kamanda amewataja waliopoteza maisha kuwa ni namba G 4467D/CPL Mussa, namba G 5702D/CPL Faraji wote askari polisi Mkoa wa Mwanza na washtakiwa Twaha Said na Tesha Murushindi waliokuwa na kesi namba P1 3/2022 kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi na mauaji.

Kamanda pia amewataja waliojeruhiwa kuwa ni PF23158A/INSP Baraka Apila, F8361 D/SGT Berison Sanga wote askari wa mkoa wa Mwanza na Maronja Katemi (52) pia amemtaja dereva wa gari, Berison Sanga mfanyakazi wa kampuni ya Nyanza Botling mkazi wa Igoma Mwanza na Paulo Charles mfanyakazi 
Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: