Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, June 1, 2022

Majeshi ya Urusi yakaribia kuukamata mji wa Sievierodonetsk, Ukraine


Ukraine imesema Urusi inakaribia kuchukua udhibiti wa karibu mji wote wa Sievierodonetsk ambao umekuwa kitovu cha kampeni ya vikosi vya Urusi ya kulimakata jimbo muhimu la Donbas mashariki mwa Ukraine. 

Gavana wa mkoa wa Luhansk uliko mji huo wa viwanda wa Sievierodonetsk amesema sehemu kubwa ya mji huo uko mikononi mwa wanajeshi wa Urusi lakini wapiganaji wa Ukraine bado wanpambana na hawajatangaza kusalimu amri. 

Wakati huo huo rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema vikosi vya nchi hiyo vimepata mafanikio fulani kwenye uwanja wa vita karibu na mji wa kusini wa Kherson na pia vinasonga mbele kwenye maeneo kadhaa ya jimbo la Kharkiv. 

Akizungumza kupitia ujumbe wa video wa kila siku Zelenksyy amesema wapiganaji wa Ukraine wanaonesha ujasiri mkubwa licha ya kupitia hali ngumu ya kulikabili jeshi la Urusi lenye mbinu za kisasa na silaha za kisasa.


Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: