Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, June 22, 2022

Sababu 5 Muhimu za Kukufanya ununue Infinix NOTE 12 VIP badala ya Samsung A53?

 


Habari wapenzi  Wasomaji wa Mpekuzi...

Leo tuangazie simu mbili za Infinix NOTE 12 VIP na Samsung A53, na mwishowe tutajua ni kwanini ununue Infinix NOTE 12 VIP badala ya Samsung A53.

Tupitie pamoja sifa za simu hizi mbili za Infinix NOTE 12 VIP na Samsung A53;

CAMERA

Tukianza na camera simu ya Infinix NOTE 12 VIP ina camera yenye MP 108 huku ikiwa na teknolojia za kisasa zaidi kufanya kukupa picha nzuri zaidi na angavu.

Sumsung A53 ina kamera yenye MP 64 ikiwa inazidiwa mbali na simu ya Infinix NOTE 12 VIP  ambayo kamera yake ni kubwa zaidi na kuifanya simu kuwa VIP.

BETRI

Kwa upande wa betri simu ya Infinix NOTE 12 VIP ina 4500mAh na teknolojia ya 120W Fast Charging, teknolojia inayoifanya simu hii kuwa simu ya kwanza kuwa na uwezo wa kujaza 100% simu ndani ya dakika kumi na saba (17 Minutes).

Na upande wa Samsung A53 ina betri ya 5000mAh ikiwa na teknolojia ya 25W Fast Charging, Teknolojia hii inauwezo wa kujaza 100% ndani ya lisaa limoja na dakika kadhaa ikiwa nyuma sana kulinganisha na 120W ya Infinix NOTE 12 VIP.

STORAGE

Infinix NOTE 12 VIP imekuja na 13GB (8GB+5GB RAM Fusion) na 256GB Room kuifanya simu ya kwanza kwenye series ya NOTE yenye room kubwa na RAM kubwa zaidi.

Samsung A53 imekuja na 8GB RAM pamoja na 256GB Room ikiwa imezidiwa RAM na Infinix NOTE 12 VIP.

BEI

Kulingana na uchambuzi huo hapo juu, moja kwa moja unaweza kusema hapo simu ghari zaidi ni Infinix NOTE 12 VIP ila ukweli ni kuwa ni tofauti, Infinix NOTE 12 VIP inapatikana kwa Tsh. 820,000/= huku simu ya Samsung A53 ikipatikana kwa Tsh. 875,000/=

Mpaka hapo tunadhani utakuwa umefahamu kwanini ununue simu ya Infinix NOTE 12 VIP badala ya Samsung A53.

Simu zote zinapatikana madukani kwa sasa, Acha comment yako hapo chini kama kuna kitu kuhusiana na hizi simu mbili ungependa kukifahamu zaidi;


Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: