Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ameipongeza Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan (AKDN) kwa mchango wake mkubwa katika kukuza na kuendeleza sekta za elimu, afya, miundombinu, utalii na utamaduni hapa nchini.
Balozi
Mbarouk ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 65 ya Uimamu wa
Kiongozi wa Kiroho wa Madhehebu ya Shia Ismailia duniani, Mhe. Karim Aga
Khan.
Balozi
Mbarouk ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo
yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo, amesema Taasisi hiyo ambayo kupitia
miradi mbalimbali iliyopo Tanzania Bara na Zanzibar ikiwemo ya elimu na
afya na ile ya kujikwamua kiuchumi imewasaidia watu wengi ambapo hadi
sasa takriban watoto 10,000 nusu ya hao wakiwa wasichana wamefaidika kwa
kupata elimu bora kupitia taasisi hiyo.
“Kupitia
uongozi mzuri wa Mheshimiwa Aga Khan, Taasisi ya AKDN imekuwa mstari wa
mbele kuchangia katika sekta za elimu, afya, maendeleo ya uchumi na
kuondoa umaskini kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Hivyo ninayo
furaha kuungana na jamii ya Ismailia ya hapa nchini na duniani kwa
ujumla kusherehekea siku hii muhimu ya miaka 65 ya Mhe. Aga Khan kuwa
Imam wa Madhehebu ya Shia Imailia” alisema Balozi Mbarouk.
Kadhalika,
Mhe. Balozi Mbarouk alisema anapongeza jitihada zinazoendelea kufanywa
na AKDN katika kuboresha huduma za afya nchini ambapo kupitia jitihada
hizo, mwezi Aprili 2022, Mkuu wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii ya AKDN,
Mhe. Zahra Aga Khan, Mkuu wa Kamati ya Jamii ya AKDN alitembelea
Tanzania na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo
cha Huduma za Saratani jijini Dar es Salaam cha kiwango cha kimataifa
ambacho kitakuwa na uwezo wa kutoa huduma mbalimbali kuhusu ugonjwa wa
saratani ikiwemo kinga, utambuzi wa mapema wa ugonjwa, matibabu na
huduma za nyumbani kwa wagonjwa .
Kwa
upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya AKDN hapa nchini, Mhe.
Balozi Amin Kurji amesema Taasisi yake itaendelea kushirikiana na
Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta mbalimbali
zikiwemo za afya na elimu. Amesema, kupitia taasisi hiyo tayari miradi
mbalimbali ikiwemo ya Vyuo Vikuu, Vyuo vya Afya vya wauguzi na wakunga
vimeanzishwa nchini.
Aidha,
ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
maendeleo makubwa ya uchumi na jamii yaliyopatikana nchini katika
kipindi kifupi tangu aingie madarakani na kwamba Taasisi ya AKDN
itaendelea kushirikiana na Serikali ili kuunga mkono jitihada hizo.
“Nampongeza
Mhe. Rais Samia na Serikali yake kwa ujumla. Tumeshuhudia uwekezaji
mkubwa unaofanywa na Serikali katika kuboresha sekta za afya, elimu
maji, umeme, miundombinu na sekta za uzalishaji. AKDN inaahidi kuendelea
kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha maisha ya
Watanzania” alisisitiza Balozi Kurji.
Maadhimisho
hayo ambayo yalifanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
yalihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, Mabalozi,
Wabunge na Wageni wengine waalikwa.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )