Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 5, 2021

Majaliwa: Rais Magufuli Amedhamiria Kuboresha Miundombinu Nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameamua kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafiri nchini ikiwemo ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa (SGR) ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 5, 2021) baada ya kukagua maendeleo ya sehemu ya kipande cha pili cha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa cha kutoka Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu ambaye amekagua kipande cha kutoka Ihumwa hadi Igandu amesema ameridhishwa na kazi nzuri inayoendelea kufanywa na amewataka wananchi wajiandae kutumia reli hiyo ambayo inajengwa kwa ajili yao.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kupunguza muda wa safari, mfano kutoka Dar es Salaam – Dodoma muda utakuwa saa tatu badala ya saa nane za sasa.

Waziri Mkuu amewataka Watanzania waliopata kazi katika mradi huo wafanye kazi kwa uaminifu na weledi wa hali ya juu ili kuudhihirishia ulimwengu kwamba Watanzania wanaajirika. “Endeleeni kuchapakazi nyinyi ni mabalozi mtakaowawezesha wengine kupata ajira.”

Amewataka Watanzania wahakikishe wanazielewa vizuri shughuli wanazozifanya katika mradi huo ili baadaye waweze kuisimamia wenyewe reli hii ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati. “Tumieni ujenzi wa mradi huu kama sehemu ya kupata utaalamu.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa kipande cha pili cha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Makutupora umefikia asilimia 56.1 na unatarajiwa kukamilika Februari, mwakani.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutashusha gharama za usafirishaji mizigo kati ya asilimia 30 mpaka 40 na kuifanya bandari ya Dar es salaam kuhimili ushindani. Kipande cha kutoka Morogoro – Makutupora chenye urefu wa kilomita 422 kinajengwa na Kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchi ya Uturuki kwa gharama ya shilingi trilioni 4.4.

 “Reli hii itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususani nchi zisizopakana na Bahari, hivyo kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa. Pia mradi huu utachochea uanzishwaji wa viwanda katika maeneo mengine ya nchi kwa kuwa utoa uhakika wa usafirishaji wa mali ghafi na bidhaa.”

Mkurugenzi huyo amesema mpaka kufika tarehe 01 Machi, 2021 mradi huu ulikuwa na wafanyakazi 8,014, ambapo 6,472 sawa na asilimia 81% ni Watanzania na 1,542 sawa na asilimia 19% ni raia wa kigeni na kwamba TRC imeendelea kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wataalamu wake mbalimbali, ambapo kwa sasa zaidi ya wataalamu 40 wanashiriki moja kwa moja kwenye ujenzi wa mradi wa SGR.


(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Read More

Naibu Waziri Ulega aziagiza Taasisi za Michezo kuboresha maisha ya Wachezaji.


 Na Grace Semfuko, MAELEZO.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega ameiagiza Idara ya Michezo ya Wizara hiyo, kukaa pamoja na Taasisi zinazosimamia sekta ya michezo nchini kujadiliana na kupata namna bora ya kuboresha maisha ya Wachezaji wakati wote wanapokuwa kazini na wanapostaafu.

Ulega amezitaja taasisi hizo kuwa ni Baraza la Michezo la Taifa- BMT, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania-SPOTANZA na kuongeza kuwa hali za maisha ya wachezaji zinapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu, kwa sababu wamekuwa na mchango mkubwa katika Taifa.

Ameyasema hayo katika kikao cha pamoja cha wadau wa Taasisi zinazosimamia michezo nchini uliojadili maslahi na namna ya kuwapata Wachezaji wapya, kuanzia ngazi za chini watakaoweza kuendeleza soka la Tanzania.

“Ninaelekeza Idara ya Michezo ya Wizara, Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Bodi la Ligi na Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania- SPOTANZA na wadhamini wetu, mkae mjadiliane kuhusu mustakabali mwema wa Wachezaji wetu ikiwa ni pamoja na huduma za afya na maandalizi ya maisha ya baada ya kustaafu soka” amesema Naibu Waziri Ulega.

Aidha, alizitaka taasisi hizo kusimamia na kuhakikisha Chama cha Wachezaji wa mpira wa miguu Tanzania SPOTANZA kinaimarika ipasavyo kwa kubuni vyanzo vya kudumu vya fedha ili kulinda maslahi ya wachezaji na mchezo wa soka nchini.

“Nawataka pia mshirikiane kwa pamoja katika kubuni vyanzo vya kudumu vya mapato, nataka kwa dhati kabisa kuona chama cha wachezaji wa mpira wa miguu kinaimarika ipasavyo, kuwe na chanzo cha uhakika ambacho kitasimamia vyema haki za wachezaji, leo hii utakuta mchezaji amestaafu lakini maisha yake yanakuwa magumu sana, hii ni kwa sababu hatukuwajengea mazingira mazuri tangu mwanzo” amesema Naibu Waziri Ulega.

Read More

Waziri Aweso Ataja Kilichokuwa Kinakwamisha Miradi Ya Maji Nchini


 Na Assenga Oscar

Waziri wa maji Jumaa Aweso amezitaja sababu zilizokuwa zikikwamisha miradi ya maji kuwa ni kutokana na kuwatumia wakandarasi wababaishaji na wasiokuwa na uwezo.

Waziri Aweso ametoa, sababu hiyo wakati akifungua kikao kazi cha wadau wa maji Mkoa wa Tanga kilichofanyika wilayani Lushoto.

Waziri Aweso alisema wakandarasi wasiokuwa na uwezo walikuwa wakipewa zabuni kwa kujuana na hivyo kusababisha kusababisha miradi ya maji kutokamilika na hatua hazichukuliwi.

Alisema wizara hiyo hivi sasa imeondokana na changamoto  hiyo baada ya kuweka mikakati ya kuhakikisha wakandarasi wa namna hiyo hawapati nafasi.

"Wataalamu walikuwa wakijua wazi kuwa baadhi ya wakandarasi walikuwa hawana uwezo lakini bado walikuwa wakiwatumia na kuwaacha wale wenye uwezo,"alibainisha waziri Aweso.

Sababu nyingine iliyokuwa ikikwamisha miradi hiyo ya maji ni michakato isiyokuwa na ulazima ambayo ilikuwa ni kikwazo kikubwa cha ukamilishaji wa miradi mbalimbali nchini.

Aliwaagiza, watendaji kayika, wizara hiyo kuacha visingizio badala yake watekeleze wajibu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameipongeza wizara hiyo ya maji kwa kujitahidi kufikisha maji katika maeneo yaliyokuwa na changamoto kubwa ya maji katika Mkoa Tanga.

Naye Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa)  Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo katika kutekeleza, bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 Ruwasa Mkoa Tanga inategemea kutumia jumla ya shilingi 38,437,802,839.39 ingawa mahitaji halisi ni shilingi 41,872,700,424.04 ili kukamilisha ujenzi wa miradi inayoendelea.

Alisema miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa miradi chakavu,  usanifu na ujenzi wa miradi mipya.

"Ruwasa Tanga inajumuisha wilaya zake 7 na inategemea kutekeleza ujenzi miradi ya mipya ya maji kukarabati ya zamani kupanua miradi inayoendelea na kusanifu miradi mipya kwa kupitia  bajeti ya mwaka wa fedha 2021/12.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kufanya tathimini pamoja na kuangalia hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwenye miradi ya maji.

Read More

Mhe. Jafo Aridhishwa Na ujenzi wa Barabara inayoingia Hospitali ya Uhuru , Dodoma


Na. Thereza Chimagu, Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb), ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Barabara inayoingia Hospitali ya Uhuru kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Mita 320 kwa njia mbili ambayo inasimamiwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Waziri Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akifanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali mkoani Dodoma Machi 03, 2021 na kuoneshwa kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Barabara hiyo.

“Tumejenga Hospitali ya Uhuru lakini sehemu hii ya kuingilia ilikuwa na changamoto kubwa, nimekuja hapa kuangalia maendeleo ya ujenzi wa barabara hii na kwa kweli nimeridhika kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hii”, alisema Mhe. Jafo.

Aidha Mhe. Jafo alimtaka Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara hiyo M/S Nyanza Co. Ltd kutumia muda uliopo ili kuweza kukamilisha mradi kwa wakati kutokana na changamoto za mvua zinazoendelea kunyesha.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara hiyo, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mhandisi Nelson Maganga alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umefikia asilimia 85 na tayari lami nyepesi imekamilika kwa ajili ya kuweka tabaka la lami nzito.

“Ujenzi wa Barabara umefikia asilimia 85 kukamilika na tunatarajia Mkandarasi kumaliza kazi kulingana na mkataba kufikia Machi 14, 2021, sehemu hii ya barabara imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 511”, alisema Mhandisi Nelson.

Katika hatua nyingine Mhe. Jafo alifanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 51.2 na kuonesha kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara hiyo Kampuni ya China Heinan International Cooperation Co. Ltd (CHICO) na kumtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anamaliza ujenzi kama ilivyo kwenye Mkataba ifikapo Julai 30, 2021.

“Sijaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huu kuwa chini ya asilimia 6, leo hii mpo asilimia 63 na mlitakiwa muwe asilimia 69 mimi nilikuja hapa nikijua mpo asilimia 70, sihitaji mjadala wa aina yeyote ninachotaka mradi huu uwe umekamilika kama ilivyo kwenye makubaliano”, alisema Mhe Jafo.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba, Mkurugenzi wa Barabara za Mijini TARURA, Mhandisi Mohamed Mkwata alisema kuwa Mkandarasi amefikia asilimia 63 za maendeleo ya jumla ya utekelezaji wa Mradi ambapo alitakiwa kuwa asilimia 69, ameongeza kuwa ujenzi wa tabaka la lami umefikia Km 11.2, uwekaji wa lami nyepesi Km 15.7, ujenzi wa tabaka la pili umefikia Km 15.7, ujenzi wa tabaka la kwanza umefikia Km 15.7, ujenzi wa mifereji Km 6.6, pamoja na ujenzi wa vivuko 64 dhidi ya 130 vinavyohitajika.

Aidha, Mhandisi Mkwata alieleza kuwa katika kipindi cha mwezi Novemba 2020 uhaba wa Saruji pamoja na mvua zinazoendelea kunyesha zilisababisha baadhi ya kazi kusimama na kufanya Mkandarasi kuwa nyuma ya asilimia 6 za utekelezaji wa Mradi na kuongeza kuwa ili kufidia muda uliopita Mkandarasi ameongeza mitambo ili kuweza kumaliza mradi huo kwa wakati uliopangwa.

Mhe. Jafo amefanya ukaguzi katika Barabara ya Mji wa Serikali Mtumba ikiwa ni ziara yake ya tatu kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo inayosimamiwa na TARURA na mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Julai, 2021.

Read More

Serikali yaonya Watu wanaotoa taarifa bila kufuata taratibu.


Na Grace Semfuko, MAELEZO.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewaonya watu na vyombo vya habari vinavyokiuka taratibu za utoaji wa taarifa kwa jamii kuhusiana na mambo mbalimbali ya Serikali na kusema kuwa, zipo mamlaka zilizothibitishwa na kwa ajili ya utoaji wa taarifa hizo.

Dkt. Abbasi amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tabia mpya ya baadhi ya vyombo vya habari, Watu na Mitandao ya kijamii, ambao wanatoa taarifa mbalimbali zinazohusu Serikali na Taasisi zake bila kuzingatia misingi ya utoaji wa taarifa hizo suala ambalo linakwenda kinyume na matakwa ya Sheriai na kuwataka kuacha hufanya hivyo.

“Sasa naona kama kuna tabia mpya imejitokeza ya baadhi ya watu, mtu anajitokeza anaanza kutoa takwimu zake kuhusu maradhi mbalimbali, kuhusu vifo, kuhusu wagonjwa, hili kwa niaba ya serikali naomba kusisitiza sio sahihi, na tuviombe vyombo vya Habari viachane kabisa na watu wa namna hiyo, kila mwanajamii asasi za kijamii mbalimbali, viongozi wa dini, wa siasa, kila mwanajamii anapaswa kushiriki katika kutoa elimu kuhusu hatua za kuepukana na kuhamasisha kuitoa jamii hofu na kusisitiza masuala yale ambayo yapo kwenye miongozo lakini masuala ya takwimu na kisera yanapaswa kubaki kwa serikali” amesema.

Amesema Serikali imekuwa ikitoa taarifa zake kwa kuzingatia taratibu na kwamba yoyote anaehitaji taarifa zozote za Serikali milango ipo wazi kabisa na kwamba wawasiliane mamlaka husika ili wapate taarifa sahihi za takwimu wanazotaka kuzitoa.

“Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tabia mpya ya baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii au maeneo mengine ya nchi kujitolea tu taarifa, zingine zikiwa zinahusu Serikali, zingine zikiwa zinahusu taasisi mbalimbali za Umma bila kuzingatia misingi ya utoaji wa Taarifa hizo, ni juzi tu Mheshimiwa Rais aliagiza viongozi mbalimbali watoe taarifa kwa umma waeleze miradi na matukio mbalimbali yanatokea katika taasisi zao, nimeona leo nisisitize tena kwamba, Serikali ina utaratibu wake wa kutoa taarifa” alisema.

Amesisitiza kuwa watu ambao hawahusiki katika agizo hili la utoaji wa taarifa zinazohusu maslahi ya umma kama magonjwa mbalimbali yakiwepo ya milipuko na mengineyo, hiyo ni kazi ya Serikali na sio ya mtu binafsi.

“Kwa hiyo watu wengine ambao hawahusiki na taratibu hizo hawapaswi kuingilia huo mfumo na hiyo itifaki  kama ilivyo kwenye maeneo mbalimbali, mfano kwenye maeneo ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa ya mlipuko, zipo taratibu za sheria ya huduma na sheria ya Afya ya jamii zimeeleza wazi kabisa kwamba ni kiongozi wa nafasi gani anaweza kutoa taarifa, lakini vilevile mfano mwaka jana Tanzania ilipopata agonjwa wa Corona, Mheshimiwa Rais alitoa itifaki ya viongozi watakaosemea ugonjwa huu, sasa mtu anapoibuka na kusema anakosea” amesisitiza.

Aidha aliwataka watu kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.


Mwisho.
Read More

AUDIO: Super Woman - Tanzanian Men All Star


AUDIO: Super Woman - Tanzanian Men All Star

Read More

Waziri Lukuvi Atangaza Uhakiki Kubaini Wamiliki Wa Ardhi Hewa Nchi Nzima


Na Munir Shemweta, ILEMELA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema Wizara ya Ardhi kuanzia tarehe 1 Julai 2021 itaanza zoezi la uhakiki la kitaifa kuwatambua na kuwaondoa  wamiliki wote hewa wa viwanja nchini.


Lukuvi alisema hayo kwa nyakati tofauti tarehe 4 Machi 2021 katika ofisi za halmashauri ya Manispaa ya Ilemela alipopokea taarifa ya utekelezaji majukumu ya sekta ya ardhi na eneo la Kigoto katika kata ya Kirumba alipogawa ankara za malipo kufuatia kuhitimishwa kwa mgogoro kati ya wananchi wa eneo hilo na jeshi la polisi akiwa kwenye  ziara ya kikazi katika mkoa wa Mwanza.


“Lazima tufanye uhakiki wa wamiliki wote wa ardhi ili kuwatambua na kuondoa wamiliki hewa, katika miji kuna maeneo mengi hayajengeki kwa sababu wamemilikishwa watu ambao hawapo” alisema Lukuvi.


Alisema, katika zoezi hilo halmashauri za wilaya zitatakiwa kuandaa jedwari la kumbukumbu za wamiliki ili zoezi hilo litakapoanza taarifa mpya zitakazojumuisha kumbukumbu zilizopo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), namba za simu pamoja na taarifa za kibenki ziingizwe.


Lukuvi alisema, wapo wananchi waliojenga katika maeneo mbalimbali majina yanatofautina na wengine  majina ya kubuni lakini  hawapo tanzania na kusisitiza kuwa ikibainika viwanja vyao vitapigwa mnada na aliwaonya  watumishi wa sekta ya ardhi kutoharibu nyaraka kutokana na kuhusika kwao kwa namna moja ama nyingine katika umilikishaji.


Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi zoezi la kutambua wamiliki wa ardhi hewa halina lengo la kunyanganya viwanja bali ni kujua wamiliki halali na kusisitiza kuwa watendaji wa sekta ya ardhi lazima wafanye zoezi hilo kwa umakini na uaminifu mkubwa.


” Najua baada ya kutangaza zoezi hili la uhakiki baadhi ya Maafisa ardhi wataanza kuhangaika kuuza viwanja na wengine kunyofoa nyaraka, tumieni njia sahihi maana kila mtu ana haki ya kumiliki kiwanja zaidi ya kimoja cha msingi ni kufuata sheria.


Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi aliwapatia ankara za malipo ya ardhi wananchi 600 wa eneo la Kigoto kata ya Kirumba katika halmashauri ya Manispaa ya Ilemela lililokuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya wananchi wa eneo hilo na jeshi la Polisi.


” Ninyi wananchi wa Kigoto wamepatiwa eneo hili na Mhe. Rais John Pombe Magufuli bila kutozwa gharama za thamani ya ardhi na ndiyo ninyi pekee katika mkoa wa Mwanza mliopata eneo kwa gharama nafuu, mmuombee  Rais Magufuli kwa kuwapatia eneo” alisema Lukuvi.


Vile vile, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitangaza kuanza awamu ya pili ya mpango wa Funguka kwa Waziri utakaowezesha wananchi wenye migogoro ya ardhi  kujaza fomu maalum na kuiwasilisha ofisi za ardhi za mikoa kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi na Waziri.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela aliwahakikishia wananchi wa Ilemela kuwa serikali itahakikisha inamaliza migogoro yote ya ardhi katika mkoa wa Mwanza kama ilivyoshughulikiwa mgogoro wa Kigoto katika kata ya Kirumba mkoa wa Mwanza.


Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza Eliah Kamyanda alisema mgogoro wa eneo hilo ulidumu kwa takriban miaka 30 mpaka mhe Rais aliporidhia wananchi hao kurejeshewa eneo hilo.


Alisema, mgogoro huo ulipitia hatua mbalimbali na kwa sasa kazi ya upimaji eneo hilo limekamilika na wananchi wapatao 600 wamepatiwa ankara za malipo ya kumilikishwa.

Read More

Tathmini Yafichua Hasara Ya Sh.bilioni 1.6 Upanuzi Hospitali Ya Tumbi


Na.Catherine Sungura,Kibaha
Uchunguzi wa tathmini ya uwepo wa thamani ya fedha katika utekelezaji wa mradi wa upanuzi na uboreshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi umeonesha hasara ya shilingi bilioni 1.6.


Hayo yamebainishwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima wakati akipokea tathmini ya awali ya mradi huo baada ya maagizo yake aliyoyatoa mnamo tarehe 24 Disemba,2020 alipotembelea hospitali hiyo na kutoridhishwa na ujenzi huo.


Katika ziara yake hiyo Dkt.Gwajima alitoa maelekezo kwa Katibu Tawala Mkoa wa kufanya tathmini ya uwepo wa thamani ya fedha  katika utekelezaji wa mradi wa upanuzi na uboreshaji wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi na hasara hiyo imebainika kwa kuhakikiwa kwa baadhi ya vipimo vya kazi na kuchukua sampuli chache kwa ajili ya vipimo vya kimaabara  jambo lililoashiria kuwepo kwa hasara kubwa zaidi Kama ingefanyika tathmini ya kina.


“Ripoti nimeipokea na iko dhahiri kabisa mahitaji ya upanuzi na uboreshaji wa hospitali ya Tumbi yalikadiriwa kutekekezwa kwa shilingi bilioni 29 baada ya Serikali kuonyesha nia ya kusaidia ufadhiri wa mradi huo kufuatia mpango wa awali wa uongozi wa Mkoa wa mwaka 2007-2009 iliokuwa na makadirio ya shilingi bilioni 5”. Alisema Dkt.Gwajima.


Aliongeza kuwa mpaka sasa jumla ya shilingi bilioni 9.4 zimekwishatolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo Kati ya shilingi bilioni 29 zilizokadiriwa ambapo bilioni 5.5 imetumika katika utekelezaji chini ya usimamizi wa Shirika la Elimu Kibaha na Katibu Tawala Mkoa na bilioni 3.9 zimehamishiwa Wizara ya Afya.


Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema kupitia taarifa hiyo imebaini kuwepo kwa mikataba ya Wakandarasi wawili SUMA JKT na MUST Construction Bureau kinyume na Sheria namba 7 ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 pamoja na marekebisho yake mwaka 2016.


“Kutokana na mkanganyiko huo namuelekeza Katibu Tawala Mkoa kupitia Kamati yako ya tathimini mfanye tathimini ya kina ndani ya siku thelathini  na kuniainishia  hasara halisi kwa kurejea vipimo vya jengo zima, kutathimini na kushauri kama jengo hili linafaa kwa matumizi ya Umma pamoja na Hali ya majengo ya zamani Kama yanafaa kukarabatiwa na kutumika Tena kwa gharama stahiki”Alisisitiza Dkt.Gwajima.


Licha ya hayo Waziri huyo aliitaka Kamati hiyo pia ihakiki uhalali wa uhitaji wa shilingi bilioni 29 katika mpango wa upanuzi kwa kurejea michoro ya mpango, kuainisha sababu zilizopelekea wizara kurudia ununuzi wa mkandarasi wa awamu ya pili A na ukidhi wa kisheria katika mchakato  huo wa kumnunua mkandarasi mpya na kuagiza mradi huo usitishwe na madeni yasiendelee kulipwa mpaka atakapopokea tathimini ya kina na kuelekeza vinginevyo.

Read More

Vijana Waaswa Kuchangamkia Fursa Ya Mikopo Yenye Riba Nafuu Inayotolewa Na Halmashauri Pamoja Na Mfuko Wa Maendeleo Ya Vijana


Vijana nchini wamehimizwa kuchangamkia fursa ya mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na Serikali kupitia makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ili waweze kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Mkoani Geita alipotembelea vikundi vya vijana ambavyo vimenufaika na mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na Halmashauri mbalimbali nchini pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya vijana, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuchangamkia mikopo hiyo yenye riba nafuu ili waweze kuanzisha miradi ya uzalishajimali kwenye jamii zinazowazunguka.

Alieleza kuwa, Serikali kupitia halmashauri zilizopo nchini zimekuwa na wajibu wa kutenga fedha asilimia 10 kupitia makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu ili viweze kuanzisha miradi mipya au kuendeleza shughuli zao ambazo zitatoa fursa ya kuzalisha ajira zaidi na kuwasaidia kujiingizia kipato na hivyo kuchangia katika kuendeleza gurudumu la maendeleo.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli imeendelea na azma yake ya kuwawezesha vijana kwa kutoa fursa nyingi kwa vijana ikiwemo mikopo yenye riba nafuu lakini vijana wamekuwa hawatumii fursa hizo zinazotolewa na serikali kwa kuanzisha miradi mikubwa itakayowawezesha kujiajiri na kuajiri vijana wenzao,” alisema Katambi

Alisema lengo la Serikali kutoa mikopo hiyo ni pamoja na kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira, hivyo kupita mikopo hiyo ambayo ina riba nafuu makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wataweza kunufaika kwa kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itawaingizia kipato na hatimaye kuweza kujikwamua kiuchumi.

Aliongeza kuwa, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma Novemba 13, 2020 alieleza kuwa Serikali imeongeza jitihada za kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba ama yenye riba nafuu ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri na pia kupitia mifuko na Programu mbalimbali zilizoanzishwa na serikali.

Sambamba na hayo alielezea pia juu ya uwezekano wa kuiunganisha baadhi ya mifuko ili ifanye kazi kwa tija zaidi kwa kuimarisha usimamizi wa mifuko hiyo na kuhakikisha watanzania wanaifahamu.

Naibu Waziri Katambi, alitaka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuangalia namna bora ya kuanzisha mpango wa kutoa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara ili kabla ya kuwapatia mkopo vijana waweze kuwajengea ujuzi utakaowasaidia kuimarisha biashara zao na kuzisimamia kwa weledi pamoja na kuwa na mbinu za kukuza biashara zao. Pia alihamaisha halmashauri kuona namna ya kuwawezesha vijana kwenye mikopo wanayoomba asilimia 50 ikawa kwa ajili ya vifaa au vitendea kazi na asilimia 50 nyingine kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli ya biashara zao watakazokuwa wakifanya.

“Kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya vijana kukosa uaminifu, wanakuja kama kikundi kukopa fedha hizo mara baada ya kuzipata wanaanza kuzitumia kwenye malengo au mipango ambayo hawakuikusudia na hivyo kushindwa kurejesha mikopo hiyo, hivyo kama kupitia mikopo waliyoomba asilimia 50 wakanunuliwa vitendea kazi au vifaa wakishindwa kuendeleza biashara itakuwa ni rahisi kwa halmashauri kuwapatia vijana wengine vifaa hivyo ambao wanaona wanaweza kufanya kazi,” alisema Naibu Waziri

Pamoja na hayo Naibu Waziri, Katambi alipongeza vikundi vya vijana alivyovitembelea ikiwemo kikundi kinachojishughulisha na uzalishaji wa Chaki kinachojulikana na jina la Rubondo na kikundi cha vijana cha Geita Youth Group kinachofatua matofali kwa hatua waliyofikia ambayo imechangia kasi ya ukuaji wa viwanda vidogo vidogo mkoani geita na ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kuongeza ukuaji wa uchumi.

Aidha, Naibu Waziri Katambi amewataka vijana kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma sambamba na kutumia maarifa waliyonayo kubuni miradi mbalimbali ya uzalishajimali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Fahil Juma alieleza kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kutoa mikopo na elimu kwa vikundi mbalimbali vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili waweze kukuza pato lao na kuongeza ajira kwa wengine zaidi.

Naye, Mnufaika wa kikundi cha Geita Youth Group, Bi. Jenifer Isaya ameishukuru Serikali pamoja na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwaamini vijana kuwa wananweza na kuamua kuwatengea mikopo hiyo yenye riba nafuu sambamba na kuwawezesha vifaa na fedha, hivyo waliahidi kuchapa kazi kwa bidi kama azma ya serikali ili warejeshe mikopo hiyo kwa wakati na kuwafanya wananchi wengine waweze kunufaika.

Mara baada ya ziara hiyo ya kutembelea vikundi vya vijana vilivyonufaika na mkopo wa asilimia nne (4) inayotolewa na Halmashauri zilizopo nchini. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi alitembelea Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sheria za Kazi pamoja na kusikiliza kero na malalamiko ya wafanyakazi kwenye maeneo mbalimbali ya kazi.

Read More

Naibu Waziri Ulega Aitaka TASCA Kubadili Katiba Yao Ili Kunufaika Na Fursa Zilizopo


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega amewaelekeza viongozi wa Umoja wa Vituo na Shule za kuvumbua, kulea na kuendeleza Michezo kwa Watoto na Vijana Tanzania (TASCA) kufanya marekebisho ya Katiba yao ili waweze kutambulika na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF) ili kunufaika na fursa zake za kuendeleza programu mbalimbali za wa watoto na vijana.

Akifanya mazungumzo na viongozi hao  Dar es salaam Naibu Waziri Ulega amewashauri viongozi hao kujisajili vitambulike kama Umoja wa Kuvumbua, Kulea na kuendeleza Mpira wa Miguu kwa Watoto na Vijana Tanzania (TAFOCA)  ili waweze kutambulika na TFF na kunufaika na fursa zake.

“Sasa usajili wa TASCA unawatambua kama Umoja wa Vituo na Shule za Kuvumbua, Kulea na kuendeleza Michezo kwa Watoto na Vijana jambo linalowakosesha fursa ya kutambuliwa na TFF,” alisema Naibu Waziri Ulega

Aidha, Naibu Waziri Ulega amewahakikishia viongozi wa TASCA kuwa Serikali imepokea mawazo yao yote ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya kuboresha Kanuni za BMT ili kuweka utaratibu wa wachezaji wa timu B za Vijana za vilabu vya Ligi Kuu na wanaofanya vizuri kwenye timu za Taifa za U17 na U20 wapewe nafasi ya kucheza kwenye michuano ya ligi Kuu badala ya kubakia kwenye timu za vijana za vilabu hivyo ili kuwaongezea uzoefu na kuendeleza vipaji vyao kwa manufaa ya Taifa.

Pia Naibu Waziri Ulega amewaahidi viongozi wa TASCA kuwa Serikali italifanyia kazi ombi lao la kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Umma kama Vyuo na Shule ili kutumia miundombinu iliyopo katika Taasisi hizo kwa shughuli mbalimbali za kukuza na kuendeleza michezo nchini.

Read More

Dampo La Pugu Kinyamwezi Limeelemewa- Waitara


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mwita Waitara amesema kuwa dampo la pugu ambalo ni dampo kuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam limeelemewa hivyo kunahaja ya kila Manispaa ya jiji la Dar es Salaam kuwa na dampo lake na kuacha kutegemea dampo la pugu ili kupunguza kero kwa wananchi walio karibu na dampo hilo.

Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa mazingira katika  jiji la Ilala Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa dampo hilo limekuwa likilalamikiwa sana na wananchi hasa kipindi cha masika, maji yanatiririka kutoka kwenye taka na kuingia katika makazi ya watu.

“Nimetembelea Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam Ubungo, Kinondoni, Kigamboni, Temeke na Nimemalizia hapa jiji la Ilala lakini nimewataka kila Manispaa wahakikishe wanadampo lao ili kuepusha adha kwa wananchi waliopo karibu na Dampo la Pugu. Hii ni njia bora ya kudhibiti kusambaa kwa taka Dar es Salaam” Waitara

Aidha Mhe. Waitara ameeleza kuwa taka zilizopo katika dampo la pugu zina changamoto zake kwani hazijatenganishwa kutoka kwenye chanzo hivyo kupelekea ugumu katika kuzichakata, ni vizuri wananchi wahakikishe wanatenganisha taka kuanzia kwenye chanzo ili kurahisisha zoezi hilo. Ameendelea kusema kuwa taka zikitenganishwa pia zinageuka kuwa fursa ya kujipatia kipato na sio taka tena

“Taka zilizopo hapa zimechanganyika kuna mifuko ya plastiki, vyuma na chupa ambavyo ingekuwa fursa katika kujipatia kipato na zisingekuwa taka tena kwani kunaviwanda vinauhitaji wa taka hizo kwa ajili ya kurejeleza. Hapa tulipofikia inabidi kuweka utaratibu ili eneo hili lianze kuwekwa miundombinu rafiki ili haya maji yasiende kwenye makazi ya watu na kusababisha kuathiri afya zao” Mhe. Waitara

Kwa upande wake Diwani wa kata ya pugu Mhe. Imelda Gerald amesema kuwa dampo kwa sasa ni kero japo meneja wa Dampo anajitahidi sana lakini kwa wananchi bado ni kero mvua inaponyesha maji machafu yanaenda kwa wananchi na kuathiri afya zao wanapata vipele, fangasi hata visima ukichimba maji yanakuwa machafu.

“Dampo la pugu limekuwa kero kwa wakazi lakini tunaomba pia magari yanayobeba taka yawe yamefunikwa ili kuepusha kudondosha taka karibu na makazi ya watu pamoja na magari yenyewe yawe mazuri maana kunamagari yanaletwa ni mabovu ambayo ni taka pia” alisema Bi Imelda

Vile vile Mhe. Waitara ametembelea Jengo jipya la Machinjio vingunguti na Machinjio ya Mazizini Gongolamboto kujionea hali ya kimazingira katika machinjio hayo. Mhe. Waitara amefurahishwa sana kuona jengo la machinjio la kisasa ambalo litakuwa rafiki kwa mazingira. Machinjio hayo bado hayajafunguliwa rasmi.

Mhe. Waitara pia alitembelea Machinjio ya Mazizini Gongolamboto na kubaini uchafuzi mkubwa wa Mazingira kwani machinjio hayo yanatiririsha maji machafu katika mfereji uliopo karibu na machinjio. Mhe. Waitara ameitaka NEMC kuchukua hatua za kisheria kuwajibisha Machinjio hayo mara moja

“Naagiza NEMC kuchukua hatua za kisheria kwa machinjio haya, kutiririsha maji katika mazingira ni kosa la kisheria hivyo wapigwe faini na onyo. Maji haya hayaruhusiwi kupelekwa kwenye mfereji au kwenye chanzo chochote cha maji bila kupimwa na kupewa kibali kutoka katika mamlaka husika” alisema Mhe. Waitara

Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya siku tano katika Mkoa wa Dar es Salaam na amefanikiwa kutembelea Manispaa zote na kutoa maagizo katika kila Manispaa.

Read More

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo March 5

Read More

Thursday, March 4, 2021

Mawaziri Watatu Zanzibar Walioteuliwa na Rais Mwinyi Hivi Karibuni Waapishwa


Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewaapisha mawaziri watatu huku wao wakiahidi kufanya kazi kwa weledi ili kuleta mabadiliko makubwa.
Read More

Waziri Mkuu Aridhishwa Na Kazi Kubwa Iliyofanywa Na Wizara Ya Kilimo Kuwadibiti Nzige mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha


 Serikali imeridhishwa na kazi inayoendelea kufanywa na viongozi wa wizara ya kilimo na wataalam wake kuhakikisha makundi ya nzige yaliyovamia mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha yanavyodhibitiwa kwa kuuwawa.


Kauli hiyo ya serikali imetolewa leo (04.03.2021) wilayani Monduli mkoa wa Arusha wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea kijiji cha Engaruka kukagua zoezi la kunyunyuzia viuatilifu kuua makundi ya nzige na kuwa amefurahi kuona kazi hiyo imefanyika kwa mafanikio chini ya uongozi wa Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda.


Waziri Mkuu aliyeambatana na Wakuu wa Mikoa wa Arusha, Manyara na Kilimanjaro alisema serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na wataalam wa wizara ya Kilimo pamoja na wale wa halmashauri za Mwanga, Siha, Longido, Simanjiro na Monduli kuwadhibiti makundi ya nzige licha ya ugumu wa mazingira ya porini.


“Nimeridhika na kazi iliyofanyika hadi sasa kuwadhibiti nzige waliovamia maeneo ya mikoa yetu ya Manyara, Kilimanjaro na hapa Arusha. Wizara ya Kilimo imechukua hatua madhubuti, endeleeni kuhakikisha wadudu hawa hawasambai kwenye mikoa ya jirani “ alisisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.


Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameagiza wizara ya Kilimo kutenga fedha katika bajeti ya mwaka 2021/22 kwa ajili ya kufufua Kitengo Cha Kilimo Anga ili kitumike kwa ajili ya kudhibiti wadudu waharibifu wakiwemo nzige kwa kuwa na vifaa na wataalam wa kutosha.


Alibainisha kuwa kwa kuwa sasa ni msimu wa kilimo, hakuna budi kwa maafisa kilimo kwenye mikoa yote nchini wakawa na utaratibu wa kufuatilia kwa karibu uwepo wa viashiria vya nzige ili kuijulisha wizara kwenda kudhibiti mapema kabla hawajasambaa kwenye maeneo ya mashamba na kuzaliana.


“Hatuwezi kuwapa nafasi nzige wazaliane hapa nchini kwani watapoteza malisho yetu na mazao ya chakula pia biashara .Nzige kwetu ni adui hatari hatupaswi kuwapa nafasi hata dakika moja, hawa tuliwasikia kwa ndugu zetu Kenya na tulitoa ushirikiano kuwaangamiza lakini wamefika nchini lazima tuwaangamize wote” aliagiza Waziri Mkuu.


Akitoa taarifa ya kazi ya kudhibiti nzige Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda alimweleza Waziri Mkuu kuwa kundi la kwanza la nzige liliingia nchini mwezi Januari wilayani Mwanga na mwezi Februari kundi jingine liliingia wilaya ya Longido na kusambaa kwenye wilaya za Simanjiro, Siha na Monduli.


Prof Mkenda alisema tayari wizara kwa kushirikiana na mikoa hiyo iliyokumbwa imefanikiwa kuangamiza makundi ya nzige kwenye wilaya ya Mwanga na Siha.


“Longido tuliangamiza makundi ya nzige lakini kundi dogo likakimbilia Monduli hapa Engaruka na kazi ya kuangamiza imeanza tunakwenda vizuri, tuna hakika tutawamaliza wote kwani tunavyo vifaa kama mabomba ya kuliza kwa mikono, helkopta na ndege maalum zinafanya kazi “ alisema Prof. Mkenda.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta alipongeza kazi inayofanywa na wizara ya kilimo kwa kuja eneo la tukio mapema ambapo Waziri na Naibu wake muda wote wamekuwa vijijini kushirikiana na wananchi kudhibiti makundi ya nzige.


Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alimweleza Waziri Mkuu kuwa vijiji vya Nondoto, Irelendeni na Engaruka wilaya ya Monduli ndipo makundi ya nzige yalipo kwa sasa na kuwa operesheni ya kuangamiza imefanyika jana na leo ha kuwa hali inaendea vema nzige wengi wamekufa.


Akihitimisha hotuba yake Waziri Mkuu aliwasihi wananchi kote ambako nzige wameonekana kutokuokota nzige waliokufa kwani wameuwawa kwa sumu inayoweza kuleta madhara kwa binadau endapo akila nzige hao.


Waziri Mkuu Majaliwa amehitimisha ziara yake ya siku moja wilayani Monduli kwa kuongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Engaruka ambapo amesema serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli itakamilisha ujenzi wa barabara ya lami toka Mto wa Mbu hadi Engaruka Monduli .
Mwisho
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasilino Serikalini
Wizara ya Kilimo
MONDULI
04.03.2021


Read More

Waziri Jafo azindua Magari Matatu Yatakayotoa Huduma Ya Tohara Katika Mikoa Minne Kanda Yaziwa


Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI amezindua magari matatu yatakayotoa huduma ya Tohara katika mikoa minne  ya kanda ya ziwa  ikiwemo Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara ambapo amesema kuwa mwanaume akipata tohara hawezi kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa asililimia 60.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Waziri huyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa magari matatu yenye thamani ya billioni 1.2 yaliyotolewa na Taasisi ya Intra Health International na kusema kuwa wale waliopata tohara wana asilimia kubwa ya kujizuia kwa kutopata maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia 60.

Aidha waziri Jafo amewataka waganga wakuu wa mikoa ya kanda ya ziwa washirikiane kwa dhati katika kuhakikisha huduma ya tohara inawafikia wanaume wakubwa na wadogo huku akiwataka kuyatunza magari hayo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya afya ustawi wa jamii na lishe kutoka TAMISEMI Ntuli Kapologwe amesema kuwa huduma ya utoaji tohara ni moja ya afua muhimu sana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi Nchini .

Naye mkurugenzi mkazi wa shirika la intra health international dr lucy Raymond amesema kuwa shirika limekuwa likitoa huduma ya tohara kwa wanaume wakubwa na wadogo kwa lengo la kuondoa maambukizi ya ukimwi na magonjwa mbalimbali huku akibainisha  wafanyakazi wa kutoa huduma  zaidi ya elfu moja wamepatiwa elimu ya kutoa huduma bora katika mikoa hiyo.

Sambamba na hayo Nuru mpuya mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa shinyanga amesema kuwa wamekuwa wakitoa huduma ya tohara huku akibainisha asilimia kubwa ya wanaume hawajapata tohara tofauti na mikoa mingine ya pwani na kusema huduma ya tohara itawasaidia wanaume wakubwa na wadogo katika mikoa ya kanda yaziwa ili kuondokana na magonjwa mbalimbali.

 KAULI MBIU ya kampeni hiyo  ni Tohara ya mwanaume “maisha ni sasa,wahi tohara,kuwa msafi,pata kinga.

Read More

Waziri Mhagama Awashukia Waajiri Wasiotekeleza Sheria Ya Ajira Na Mahusiano Kazini


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amekerwa na waajiri nchini wasiotekeleza Sheria na.6 ya mwaka 2014 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019, sheria hiyo inamtaka mwaajiri kumpa mkataba wa ajira mfanyakazi pamoja na kutoa haki ya kuwa na vyama vya wafanyakazi.

Waziri Mhagama akiwa katika ziara ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula kwenye viwanda vikubwa vya usindikaji wa chakula (Unga wa ngano, unga wa mahindi na mafuta ya kula) jijini Dar es salaam, wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited pamoja na Kampuni ya Unique Consultants Services, wamejitokeza kueleza kero zao zilizojikita kwenye mikataba ya ajira, kutokuwepo na haki ya vyama vya wafanyakazi, kima cha mshahara pamoja na michango yao kutopelekwa NSSF.

“Afisa kazi mkoa wa Pwani  nakupigia hii simu nikiwa hapa kwenye kiwanda cha Neelkanth Salt Ltd nataka kesho uje hapa na timu yako nataka mkague mikataba, hakikisheni kinaundwa chama cha wafanyakazi, angalia mishahara  na posho zinazingatia kazi wanazofanya, angalieni vitendea kazi. Huyu mwekezaji anafanya kazi nzuri hapa nchini na amewekeza hadi Tanga, lakini tunataka uwekezaji wenye tija uendane na kazi zenye staha kwa watanzania” Amesisitiza Mhe. Mhagama.

Baada ya kuongea na wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services, Waziri Mhagama alipiga simu hapo hapo na kumwelekeza Afisa kazi wa mkoa wa Dar es salaam ndani ya saa moja kuhakikisha anafanya ukaguzi wa ghafla kuwasikilza wafanyakazi hao kero zao.

“Watanzania wanao wajibu wa kutafuta haki zao mahala pa kazi, nataka Afisa kazi Dar e salaam uje hapa na meneja wa Tawi wa NSSF, kwani nimeelezwa wafanyakazi hawa kwa miaka miwili michango yao ya mishahara haipelekwi NSSF.Pia nipewe taarifa ya utekelzaji wa suala hili mara moja likikamilika. Niwatake wafanyakazi mtulie serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ipo tayari kushughulikia kero za wananchi kwa wakati” Amesema Mhagama.

Katika hatua nyingine, Waziri Mhagama amewataka waajiri kuhakikisha michango ya mishaha ra ya wafanyakazi inapelekwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mujibu wa sheria. Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii sura na. 50 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2018, inakata mwajiri awasilishe michango ya wafanyakazi kwenye mfuko huo kila mwenzi ambapo mwajiri  na mwajiriwa kila mmoja huchangia 10% ya mshahara.

Read More

IGP Sirro Awataka Waendesha Pikipiki Kufuata Sheria


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya na kuwataka vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, kufuata sheria na alama za barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa Kiwangwa mkoani Pwani na kuzungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Tanga, ambapo amesema kuwa, karibu asilimia 90 ya vifo nchini vinatokana na ajali za pikipiki.

Hata hivyo, IGP Sirro amewataka wananchi hususan vijana kuacha kujihusisha na uhalifu wa kutumia silaha, wizi wa mifugo na mazao na kuwataka kujihusisha na biashara halali hasa za ujasiriamali.

Akiwa mkoani Tanga, IGP Sirro amefanya ukaguzi wa eneo la uwanja wa mbinu za medani lililopo Mkomazi mkoani humo na kusema kuwa, jitihada kubwa zinaendelea kufanyika ikiwemo kujenga majengo ya kisasa  kwa ajili ya kufanya mafunzo ya utayari kwa askari wa Jeshi hilo.

Read More

Vikao Vya Kamati Za Bunge Kuanza Tarehe 8 Hadi 26 Machi 2021

Read More

UN yaitaja siku ya jana kuwa mbaya zaidi Myanmar baada ya mapinduzi ya jeshi, raia 38 wapigwa risasi


Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Myanmar ametangaza kuwa Jumatano ya jana ilikuwa siku mbaya na ya umwagaji mkubwa zaidi wa damu nchini humo baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali ya kiraia tarehe Mosi Februari mwaka huu.

Christine Schraner Burgener amesema hayo baada ya jeshi la Myanmar kuua waandamanaji wasiopungua 38 wanaopinga mapinduzi ya jeshi jana Jumatano pekee.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa amesema, mpaka sasa watu zaidi ya 50 wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wengi wamejeruhiwa tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mapema mwezi uliopita nchini Myanmar.

Jeshi la Myanmar limewafyatulia risasi hai waandamanaji hao siku moja tu baada ya nchi jirani kutoa wito wa utulivu na kutangaza kuwa, ziko tayari kusaidia juhudi za kutafuta suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo.

Tarehe Mosi mwezi wa Februari jeshi la Myanmar lilitwaa madaraka ya nchi baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo, Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi mkubwa, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo. Jeshi la Myanmar pia limetangaza hali ya hatari ya kipindi cha mwaka mmoja na kukomesha utawala wa kiraia uliotawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 10.

Tangu wakati huo mamilioni ya Wamyanmari wamekuwa wakifanya migomo na maandamano ya nchi nzima wakipinga hatua ya jeshi ya kutwaa madaraka ya nchi.


Read More

Vijiji 52 kunufaika na mradi wa kutoa ajira za muda kwa walengwa wa Tasaf Simiyu


 Samirah Yusuph.

Itilima. Wananchi wa Wilaya ya itilima mkoani Simiyu wanatarajia kunufaika na Mradi wa kutoa ajira za muda kwa walengwa wa TASAF chini ya mpango wa kunusuru kaya masikini katika awamu ya tatu kipindi cha pili.

Mradi umelenga kuvifikia vijiji 55 kati ya vijiji 102 vya wilaya hiyo, ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita katika kila kijiji hali itakayo sababisha walengwa wa eneo husika kupata ajira za muda kwa kipindi chote cha mradi.

Hayo yameelezwa na afisa ufuatiliaji TASAF Wilaya ya Itilima Paulo Tibabihilila wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa timu ya wawezeshaji ngazi ya mamlaka ya eneo la utekelezaji kuhusu maandalizi, utekelezaji na usimamizi wa mradi.

Amesema kuwa zoezi la kuibua miradi katika vijiji limeanza katika hatua ya awali ya mafunzo kwa wawezeshaji ili waweze kwenda kubaini miradi itakayokuwa na tija  katika jamii na kuwa utekelezaji wake utatumia teknolojia rahisi pamoja na nguvu kazi ya wananchi.

"Miradi itaibuliwa na wananchi wenyewe, wataitekeleza katika hatua zote za utekelezaji na baada ya kukamilika wataisimamia...

Lengo likiwa ni kutengeneza miundo mbinu mizuri katika jamii pamoja na kuwapa wananchi ujuzi katika kuendesha miradi ili waondokane na umasikini".

Akielezea miradi ambayo itakwenda kutekelezwa katika vijiji mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo Skay Thomas amesema kuwa miradi itakayokwenda kutekelezwa ni pamoja na miradi ya upandaji miti, miradi ya maji, barabara, umwagiliaji pamoja na kuongeza rutuba ya udongo.

Huku baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Maiko Mhoja na Mary Boniphace wakieleza kuwa mradi huu umekuwa na mapokeo chanya kwa sababu umelenga kuinufaisha jamii.

"Muhimu ni kupeleka elimu katika jamii ili waweze kuwa tayari kuipokea na kuiendele za miradi kwa manufaa yao".  

Aidha mkurugenzi mtendaji wa halshauri ya wilaya ya Itilima Elizabeth Gumbo Amewataka wawezeshaji kwenda kuibua miradi endelevu katika vijiji ili hata baada ya mradi kuisha wananchi waendelee kuwa na uwezo wa kuiendeleza miradi hiyo.

Halmashauri ya wilaya ya Itilima ni miongoni mwa halmashauri 51 nchini ambazo zinanufaika na mradi wa ajira kwa muda, mlengwa atapata nafasi ya kuajiriwa kwa kipindi cha miezi sita, katika siku 30 za mwezi atafanya kazi siku 10 kwa masaa manne kwa siku.


Mwisho.

Read More

Waziri wa nishati Dkt Medadi Kalemani Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Bariadi


Samirah Yusuph,
Bariadi. Waziri wa nishati Dkt Medadi Kalemani ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovolti 220 na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Imalilo wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu wenye gharama ya bilioni 75.

Katika uwekaji wa jiwe hilo  Machi 03, Kalemani ameagiza kukamilika kwa mradi huo katika kipindi cha miezi tisa hadi kumi na mbili ili kuwawahishia wananchi huduma ya umeme wa uhakika ambayo ilikuwa haipatikani kwa muda mrefu.

Ambapo amelitaka shirika la umeme nchini Tanesco kuhakikisha kuwa litandaza mtandao wa nguzo za umeme katika maeneo yote vijijini ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata umeme majumbani.

"Zoezi la uwekaji wa umeme majumbani kwa sasa sio suala la hiali badala yake ni jambo la lazima ni kila mwananchi awe na umeme katika makazi yake...

Serikali imetumia gharama kubwa kujenga miradi hii hivyo yule atakayeshindwa kuvuta umeme nyumbani kwake tutamtafuta aseme ni kwa nini ameshindwa kuweka umeme".

Aidha aneagiza kuwa Kwa sasa mita zote za umeme katika mitaa na vijiji vitauzwa kwa bei moja bila kujali umbali wa kaya na nguzo hata walio nje ya mita 30 za nguzo watapata umeme kwa bei elekezi ambayo ni tsh 27,000.

Akitoa taarifa ya shirika la umeme mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Tito Mwinuka, amesema kuwa ujenzi wa mradi huo umegharimu kiasi cha bilioni 75 pamoja na bilioni 46.7 kwa ajili ya fidia kwa wananchi waliopisha eneo la Mradi.

"Tayari wananchi wameanza kupewa stahiki zao kama fidia baada kupisha mradi huu".

Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amesema kuwa ujenzi wa mradi huo katika Mkoa wa Simiyu utapelekea upatikanaji wa umeme kuwa wa uhakika tofauti na ilivyokuwa awali.

"Uwepo wa umeme wa uhakika katika Mkoa wetu inakwenda kuwa chachu ya kuinua uchumi wa wananchi kwa sababu wananchi wa mkoa huu ni wakulima, kupitia kulimo wataweza kulima kisasa kwa kutumia mashine ambazo zinahitaji Kumia umeme ikiwa ni pamoja na usindikaji wa mazao jambo ambalo litaongeza tija katika kilimo.

Aidha ameongeza kuwa ni wakati wa shirika la umeme kuboresha miundo mbinu ikiwamo nguzo za umeme zilizo choka ili kuhakikisha umeme haukati mara kwa mara na kuwapa adha wananchi.

Hapo awali Mkoa wa Simiyu haukuwa na kituo cha kupoza, kupokea na kusafirisha umeme badala yake ulipokea umeme kutoka katika vituo vya kupozea umeme kutoka Mwanza na Shinyanga kwa sasa kituo hiki kitakuwa na uwezo wa kufua kilowati 100 za umeme mara mbili ya hitaji la umeme kwa Mkoa.

Mwisho.

Read More

Waziri Lukuvi Aamuru Kufutwa Hati Ya Ardhi Na Kushusha Neema Kwa Wakazi Wa Mhandu Nyamagana


 Na Munir Shemweta, NYAMAGANA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameshusha neema kwa wakazi wa kata ya Mhandu katika halmashauri ya manispaa ya Nyamagana mkoa wa Mwanza kwa kuamuru kuondolewa katika daftari Hati ya kitalu Na 153 eneo hilo na kupatiwa wananchi 74 waliokuwa katika mgogoro.


Akitoa uamuzi huo tarehe 3 Machi 2021 katika wilaya ya Nyamagana alipokwenda kutatua mgogoro wa eneo hilo uliodumu kwa takriban miaka 14, Waziri Lukuvi alisema, hati ya mtu anayedaiwa mmiliki wa eneo hilo anayetambulika kwa jina la  abdallah maliki ilitakiwa kufutwa muda mrefu kwa kuwa hajalipia kodi ya pango la ardhi kwa miaka 15.


“Hati miliki ikaondolewe katika daftari la hati na jaji amethibitisha katika maamuzi yake kuwa wamiliki wa asili katika eneo hili hawakulipwa fidia” alisema Lukuvi.


 Waziri wa Ardhi aliongeza kuwa, kutokana na maamuzi hayo sasa wananchi wa eneo hilo watatakiwa kupimiwa kulingana na ukubwa wa eneo wanalomiki na kila mmiliki atatakiwa kulipa tozo la mbele (Premium) asilimia 2.5 kufidia gharama ambayo mmiliki wa awali alishindwa kulipa kodi ya pango la ardhi.


“Huyu mtu ameshindwa kuendeleza kwa wakati na hajalipa kodi kwa miaka 15 sasa wananchi wapimiwe na kupatiwa eneo bila fidia. Huwezi kupewa eneo una hati watu sabini wanajenga miaka 15 wewe una hati umekaa nayo tu” alisema Lukuvi.


 Kwa mujibu wa Lukuvi Serikali itahakikisha inalinda hati ya mmiliki wa ardhi huku mmiliki akitakiwa kulinda eneo lake na kusisitiza kuwa hati ya ardhi ni dhamana na ndiyo inayotoa usalama wa mmiliki.


 ‘Mtu hajaonekana halafu atoe kibali cha kuvunja nyumba. Sheria hairihusu umilikishaji juu ya hati nyingine ndiyo maana nimeamua kuifuta kwanza hati hii ndiyo hati nyingine isajiliwe” alisema Lukuvi.


Aidha, aliagiza eneo lingine kitalu 154 linalokaliwa na wananchi 40 na  kumilikiwa na Abdulkarim Mbaga  mmiliki wake apelekewe ilani ya siku 90 kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi ya eneo lake.


Akiwasilisha mgogoro huo mbele ya Waziri wa Ardhi mwakilishi wa wananchi wa Kata ya Mhandu Sokoni Bw. Kazimiri Shimbi alisema kuwa, muda mrefu wananchi wa eneo hilo wamekuwa katika mgogoro wa ardhi wakishitakiwa na mtu wasiyemjua jambo lililosababisha kushindwa kurasimishiwa makazi katika eneo hilo kwa madai ya kuvamia eneo. Hata hivyo, kwa mujibu wa Shimbi wananchi hao wa Mhandu mara kadhaa wamekuwa wakishinda kesi mahakamani dhidi ya mdai.

Read More

Dkt. Abbas: Watendaji Bmt Badilikeni Vinginevyo Mtabadilishwa


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amewataka watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kufanyakazi kwa bidii na wale watakaoonekana kushindwa kutekeleza majukumu yao Serikali itaawachukulia hatua ikiwa ni pamoja kuwaondoa.

Dkt Abbasi ameyasema hayo Machi 03,2021  jijini Dar es Salaam alipofanya vikao vya kukagua utekelezaji wa kazi na maagizo ya viongozi kwa Baraza  hilo pamoja na pia  Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA).

“Katika siri sita za mageuzi na mafanikio ambazo nimekuwa nikiwaeleza siku zote ni kuwa na timu yenye ari, maadili na inayojituma, hili kwa  watendaji ni jambo la muhimu sana katika Serikali yetu ya kimageuzi kufanikiwa katika  malengo ya kuivusha Tanzania,  na  hapa BMT wapo watu kama hawajaelewa hili,” alisema Dkt. Abbasi.

Katibu Mkuu Dkt. Abbasi ameongeza kuwa kuna baadhi ya hatua zimeanza kuchukuliwa kutokana na utendaji mbovu akiwemo  aliyekuwa Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo.

“Mtendaji Mkuu pendekeza ndani ya siku saba mtu mwingine wa Kukaimu nafasi hiyo ulete wizarani, huyu Msajili aliyekuwepo hapa amesharejeshwa kwenye majukumu ya taaluma yake.”alisisitiza Dkt.Abbasi

Aidha, Dkt. Abbasi alitumia kikao hicho  na BMT kuonya baadhi ya watendaji akiwemo mmoja wa watumishi wa Idara ya Utawala katika Baraza hilo kuwamua kubadilika la sivyo   atabadilishwa.

“Wizara inapokea malalamiko mengi kuhusu utendaji wako sasa inawezekana ni majungu au kweli una tatizo. Kazi ya Idara ya utawala ni kufanikisha mambo sio kukwaza watumishi na kuwatengenezea jakamoyo. Sasa wewe nilikuwa niondoke na wewe leo, lakini ngoja tukupe muda kukuangalia zaidi.”Dkt. Abbasi

Hata hivyo, awali Dkt. Abbasi alizungumza na Menejimenti ya COSOTA ambapo alisisitiza watendaji hao kukamilisha maboresho ya mifumo yanayoendelea,  ili wasanii na wabunifu wengine waanze kupata migao yao huku akisisitiza moja ya nguzo kuu za Wizara kwa sasa ni pamoja na kuona utawala na utendaji bora kuanzia Wizarani, taasisi hadi kwa wadau wa sekta zote.

“Wizara ikiongozwa na Mhe. Waziri wetu Innocent Bashungwa na Naibu wake Abdallah Ulega kwa sasa katika nguzo muhimu za mageuzi katika sekta zetu nne tumekubaliana hili la utawala bora kuanzia Wizarani, kwenye Taasisi na hadi kwenye asasi za wadau wetu ni muhimu na tutalisimamia ipasavyo. Zama za uzembe, majungu, mizungu na watu kuwekeza katika fitna na akadabraha zimekwisha. Tunanyoosha mambo, kila mtu alipo anyooke kabisa kabla hatujafika kumnyoosha.” Aliendelea kusisitiza Dkt. Abbasi.

Read More